Habari za hivi punde! Jose Mourinho apigwa kalamu na Tottentham

Muhtasari

• Mourinho amekuwa mkufunzi wa timu hiyo kwa miezi 17 pekee. 

Jose Mourinho
Jose Mourinho
Image: Getty Images

Jose Mourinho ameitimuliwa kama meneja wa tmu ya Tottenham Hotspurs.

Mourinho amekuwa mkufunzi wa timu hiyo kwa miezi 17 pekee. 

Mourinho aliteuliwa kuwa meneja wa Tottenham Hotspurs Mwezi Novemba mwaka 2019 baada ya aliyekuwa meneja Mauricio Pochettino kutimuliwa kutokana na msururu wa matokeo duni.

spurs
spurs

Meneja huyo wa zamani wa Chelsea na Manchester United alikuwa ametia kandarasi ya hadi msimu wa 2022-2023.

Tottenham kwa sasa inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la ligi ya primia huku ikiwa na matumaini finye mno kufuzu kwa dimba la mabingwa barani ulaya msimu ujao.