MAAMUZI JUJA

Mwanawe marehemu Waititu amuonya Moses Kuria

Kuria ametuhumiwa kukejeli mjane na wanawe. Adaiwa kuhudhuria mazishi kuhakikisha kweli Waititu kaaga.

Aliyekuwa mbunge wa Juja Francis Waititu
Picha na File
Muhtasari

•Munyua adai kuwa Kuria alihudhuria mazishi kuhakikisha tu kuwa Waititu kweli ameaga

•Asema Kuria ni aibu kwa jamii na wanaume wote waliokomaa

Mwanawe aliyekuwa mbunge wa Juja marehemu  Francis Waititu almaarufu ‘Wakapee’ amemkashifu Moses Kuria kwa kile anachosema ni kumkosea heshima marehemu Waititu.

Michael Munyua Waititu amemkashifu  mbunge huyo wa Gatundu ya Kusini kwa kukejeli mama yao kutokana na hamu yake ya kutaka kurithi kiti kilichoachwa wazi na marehemu mumewe. Amemsuta Kuria kwa kile anachosema ni kukejeli wajane.

Kupitia kwa wakili Wahome Thuku, Munyua amemtetea mama yake anayegombea kiti na tiketi ya Jubilee kwa kusema kuwa anatazamia kulinda sifa nzuri za uongozi alizoacha Wakapee. Amemtaja marehemu babake kuwa mwanasiasa aliyekuwa na heshima na nguvu kubwa kwenye ulingo wa siasa.

Susan Njeri, mjane wa aliyekuwa mbunge wa Juja Francis Munyua.
Susan Njeri, mjane wa aliyekuwa mbunge wa Juja Francis Munyua.
Image: JOHN KAMAU

“Ulikuja mazishi nyumbani ukijifanya kumuomboleza baba yetu aliyekuunga mkono kwenye siasa ila kwa kweli ulitaka kujihakikishia mwenyewe kwamba kweli amefariki!” Munyua alimsuta Kuria.

Mwanawe marehemu alisisitiza kuwa mama yake, Susan Njeri, ameshikilia familia imara na kamwe hawatatishiwa na siasa zake hafifu.

Hapo awali  kupitia chapisho la Facebook, Kuria alikuwa amedai kuwa sio sharti Bi Njeri kurithi cha ubunge cha Juja kwa kuwa tu ni mjane wake  marehemu Waititu.

Munyua amemsema Kuria kuwa aibu kwa jamii na wanume waliokomaa. Amemwagiza kujikomboa kabla ya kupokea apizo.