Covid-19:Watu 161 wapatikana na corona,113 wapona, 14 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 14 waaga dunia kutokana na corona,113 wapona
  • Kati ya visa hivyo 158 ni wakenya huku 3 wakiwa raia wa kigeni, pia 81 ni wanaume huku 80 wakiwa ni wagonjwa wa kike
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 91

Kenya imerekodi visa 161 vipya vya maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 2,805 zilizopimwa chini ya saa 24.

Kati ya visa hivyo 158 ni wakenya huku 3 wakiwa raia wa kigeni, pia 81 ni wanaume huku 80 wakiwa ni wagonjwa wa kike.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 91.

Kufikia leoo kenya imesajili idadi jumla ya 175,337 visa vya maambukizi ya cocona, kutoka kwa jumla sampuli ya 1,866,825.

Kulingana na twakimu za wizara ya afya watu 177 wamepona corona na kufikisha idadi jumla ya 120,208 ya watu waliopona corona.

Watu 113  wamepona huku wakipokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 64 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kuna wagonjwa 957  waliolazwa hospitalini huku wagonjwa 4,796 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Watu 14 wameaga dunia kutoka na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 3,410 watu walioaga dunia.

Vile vile kuna wagonjwa 155 ambao wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi ICU.

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya kwanza imefika 986,881 huku idadi ya waliopokea chanjo ya pili ikifika 126,277.