Mahakama yazuia vyombo vya habari kuripoti kuhusu kesi ya mtoto inayomkabili spika Lusaka

Hakimu mkazi wa Nairobi F.Terer alikubali ombi lawakili Omari na kuzuia vituo vyote vya radio, televisheni, gazeti na kidijitali kuripoti kuhusiana na kesi ile.

Muhtasari

•Kesi hiyo ilikuwa iendelee siku ya Jumanne huku mahakama ikitarajiwa kujua kama kwamba maafikiano yalikuwa yamepatikana kufuatia  majadiliano kati ya upande wa Lusaka na mwanamke mlalamishi.

•Awali mwezi huu Lusaka alikuwa amekiri kuwa ndiye mwenye ujauzito ambao mwanamke aliyemshtaki amebeba. Alikuwa amedai kuwa hana nia ya kupinga kuwa ndiye baba wa mtoto huyo. 

Spika wa Seneti Ken Lusaka. Picha: HISANI
Spika wa Seneti Ken Lusaka. Picha: HISANI

Habari na Annette Wambulwa

Mahakama imezuia vyombo vya habari kuchapisha habari zozote kuhusiana na kesi ya uzazi na ulezi wa mtoto inayomkabili spika wa seneti Kenneth Lusaka.

Wakili wa mwanamke aliyemshataki spika Lusaka Danstan Omari amepata agizo linalozuia vituo vyote vya habari kuripoti chochote kuhusiana na kesi inayoendelea.

Hakimu mkazi wa Nairobi F.Terer alikubali ombi lawakili  Omari na kuzuia vituo vyote vya radio, televisheni, gazeti na kidijitali kuripoti kuhusiana na kesi ile.

Kesi hiyo ilikuwa iendelee siku ya Jumanne huku mahakama ikitarajiwa kujua kama kwamba maafikiano yalikuwa yamepatikana kufuatia  majadiliano kati ya upande wa Lusaka na mwanamke mlalamishi.

Awali mwezi huu Lusaka alikuwa amekiri kuwa ndiye mwenye ujauzito ambao mwanamke aliyemshtaki amebeba. Alikuwa amedai kuwa hana nia ya kupinga kuwa ndiye baba wa mtoto huyo. 

Lusaka kupitia wakili wake alidai kuwa majadiliano kati yake na mwanamke huyo yalikuwa yanaendelea wakitarajia kupata suluhu nje ya mahakama.