INADAIWA LUSAKA ALITAKA MWANAMKE HUYO AAVYE MIMBA

Spika Lusaka ashtakiwa kwa tuhuma za 'kuruka mimba'

Kulingana na wakili Danstan Omari, Lusaka amekuwa na uhusiano wa karibu na mwanamke huyo na wamekuwa wakishiriki katika tendo la ndoa kuanzia mwaka wa 2018.

Muhtasari

•Mwanamke huyo amemtaka spika kumkubali mtoto huyo kuwa wake na kuwajibika katika shughuli zote za uzazi.

•Omari amedai kuwa mlalamishi amekuwa akishuhudia matatizo ya mimba kwani hana fedha za kugharamia bili za hospitali nzuri zinazohakikishia wanawake wazito huduma za hali ya juu.

Spika wa seneti Ken Lusaka
Spika wa seneti Ken Lusaka
Image: Maktaba

Mwanamke mmoja amefika mahakamani kumshtaki spika wa seneti, Ken Lusaka, kwa kutelekeza anayedai kuwa mwanawe ambaye hajazaliwa.

Mwanamke huyo amemtaka spika kumkubali mtoto huyo kuwa wake na kuwajibika katika shughuli zote za uzazi.

Kulingana na wakili Danstan Omari, Lusaka amekuwa na uhusiano wa karibu na mwanamke huyo na wamekuwa wakishiriki katika tendo la ndoa kuanzia mwaka wa 2018.

Hata hivyo, Omari amesema kuwa wawili hao walizozana miezi miwili iliyopita baada ya mwanamke yule kumfahamisha Lusaka kuwa alikuwa ameshika mimba yake kufuatia matendo yao ya  kushiriki mapenzi bila ulinzi.

"Wawili hao walizozana kufuatia agizo la Lusaka kumtaka aavye mimba ile, pendekezo ambalo mlalamishi alikataa. Kwa sasa ako na mimba ya zaidi ya  miezi mitatu kuanzia wakati alipogundua kuwa amebeba mtoto wa Lusaka kwani hajakuwa akishiriki mapenzi na mwanaume yeyote mwingine, jambo ambalo limethibishwa na  vipimo vya kidaktari" ripoti ya mahakama ilisoma.

Ripoti hizo zinaashiria kuwa licha ya kuwa na mapato makubwa, Lusaka amekataa kushughulikia bili za kliniki ili kufanikisha kukua vizuri kwa mtoto yule  ndani ya tumbo ya mamake . Inasemekana kuwa ana nia ya kumsababishia mwanamke yule msongo wa mawazo, jambo ambalo linaweza sababisha kuharibika kwa mimba.

Omari amedai kuwa mlalamishi amekuwa akishuhudia matatizo ya mimba kwani hana fedha za kugharamia bili za hospitali nzuri zinazohakikishia wanawake wazito huduma za hali ya juu.

Amedai kuwa Lusaka amekanusha uhusiano wowote naye na amekataa kukubali vipimo vya kubainisha madai hayo.

Omari amedai kuwa mlalamishi hana kazi na kwa kuwa amebeba mimba ya mtoto ambaye huenda akawa spika wa seneti kama babake , kutunzwa kwake ni kwa umuhimu mkubwa sana na kunafaa kupewa kipaumbele

Jaji James Makau amefanya dharura kesi hiyo katika kikao kilichofanyika asubuhi ya Jumatatu na kuamuru kesihiyo kusikizwa mnamo Julai 7.