Covid-19:Idadi jumla ya watu walioaga dunia imefika 4,600 baada ya watu 36 kuaga dunia

Muhtasari
  • Watu 1,258 wamepatikana na ya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,868 chini ya saa 24 zilizopita
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 232,052 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 12.8%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Watu 1,258 wamepatikana na ya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,868 chini ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 232,052 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 12.8%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 1,203 ni wakenya ilhali 55 ni raia wa kigeni,611 ni wanaume huku 647 wakiwa wanawake.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,366,466.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 6, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 98.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 36 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,600 ya walioaga dunia.

Vile vile  watu 753 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 216,127, 530 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 223 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,941 ambao wamelazwa hospitalini, 8,126 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 153 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,585,664.

 

 

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe