Kijana aua nduguye mkubwa kwa mshale kufuatia mzozo uliohusisha urithi wa mizinga ya nyuki, Baringo

Muhtasari

•Alex Kalemaa Kiptoi (18) anadaiwa kuua ndugu yake Josep Kipsingor Kiptoi (43)  kwa kutumia mkuki ambaye alishutumu kuchukua sehemu kubwa ya mizinga ya nyuki zaidi ya 40 ambayo baba yao aliwaachia

crime scene 1
crime scene 1

Polisi katika kaunti ya Baringo wanazuilia kijana mmoja anayeaminika kuua ndugu yake mkubwa kufuatia mzozo uliohusisha urithi.

Alex Kalemaa Kiptoi (18) anadaiwa kuua ndugu yake Josep Kipsingor Kiptoi (43)  kwa kutumia mkuki ambaye alishutumu kuchukua sehemu kubwa ya mizinga ya nyuki zaidi ya 40 ambayo baba yao aliwaachia.

Maafisa wa DCI wameripoti kwamba Kalemaa alimdunga Kipsingor kwa mshale kwenye paja la kushoto wakiwa nyumbani kwao katika kijiji cha Kapndasum, eneo la Koituimet baada ya kulalamika kuwa nduguye alimnyima haki yake ya urithi.

Jeraha la mshale ambalo Kipsingor alipata lilivunja damu hadi akaaga na kuwaacha wanakijiji waliofika kwenye eneo la tukio wakiwa wamejawa na mshtuko kufuatia mauaji hayo.

Polisi kutoka kituo cha Mogotio walipopokea ripoti walifika kwenye eneo la tukio na kulichambua kisha kumtia mshukiwa pingu. Baadhi ya ushahidi wa muhimu ulichukuliwa ili kutumika mahakamani.

Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika mochari moja mjini Eldama Ravine.