Huduma za Mpesa kukatizwa Jumamosi usiku

Muhtasari

• Huduma za Mpesa hazitakuwepo siku ya Jumamosi tarehe 6/11/2021 kuanzia saa sita kasoro dakika moja usiku hadi Jumapili saa kumi asubuhi.  

Afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa akizindua programu ya M-Pesa mnamo Juni 23, 2021. Picha: Twitter / Safaricom
Afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa akizindua programu ya M-Pesa mnamo Juni 23, 2021. Picha: Twitter / Safaricom

Huduma za Mpesa hazitakuwepo siku ya Jumamosi tarehe 6/11/2021 kuanzia saa sita kasoro dakika moja usiku hadi Jumapili saa kumi asubuhi.  

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricon imetangaza kwamba wakati wa kipindi hiki huduma zote za Mpesa zikiwemo kuweka salio za maongezi hazitakuwepo. 

Katika taarifa kampuni hiyo ilisema kwamba sababu za hatua hii ni kutoa nafasi kwa wahandisi kukarabati na kuboresha mifumo ya huduma zake. 

Kampuni hiyo ilisema ilichagua kufanya ukarabati huo nyakati za usiku wakati ambapo shughuli hamna shughuli nyingi za wateja wake kutumia huduma za Mpesa.