•Wachuuzi wa ngono nchini Uingereza waliandamna dhidi ya mauaji ya Agnes Wanjiru yanayodaiwa kutekeleze na mwanajeshi wa Uingereza.
Wachuuzi wa ngono afanyabiashara wa ngono katika nchi ya Uingereza wameandamana kufuatia madai ya mauji ya Agnes Wanjiru na mwana jeshi wa Uingereza.
Mnamo Disemba 17, Makundi ya mahakaba yalikusanyika nje ya afisi ya Wizara ya Ulinzi ili kuitaka haki itendeke kwa Wanjiru
Muungano wa Uingereza wa Makahaba, Kundi la Wanawake wote wa Afrika, lile la Wanawake dhidi ya Ubakaji, SWARM, walikuwa miongoni mwa makundi yaliyotaka haki itendeke kwa Agnes na wafanyakazi wengine ambao sauti zao hazikusikika.
"Tunawaheshimu na kuwaomboleza wahudumu wa biashara ya ngono duniani kote ambao wamekuwa wahasiriwa wa dhuluma na mauaji. Leo pia ni siku ya upinzani - tuko nje ya Wizara ya Ulinzi kutoa wito wa haki kwa Agnes Wanjiru, mchuuzi fanyakazi wa ngono wa Kenya na mama aliyeuawa na afisa wa Jeshi la Uingereza," baadji ya mahakaba wa Uingereza waliandika kwa mtandao wao wa twitter.
Waandamanaji walibeba bendera, mabango na miavuli vikiwa na sheheni maneno yenye kuonyesha kughadhabishwa kwao na mauaji ya Wanjiru.
Mwili wa Wanjiru ulipatikana katika Lion court Hotel, Nanyuki baada ya miezi mbili ya kutafutwa.