Kanze Dena amtetea rais Kenyatta, asema amefanya maendeleo

Muhtasari

• Msemaji wa ikulu, Kanze Dena amemtetea utendakazi wa rais Uhuru Kenyatta akisema kwamba sehemu alizofeli zilikuwa nje ya uwezo wake.

• “Rais ni binadamu tu, wewe utahisi vipi wakati umefanya kazi na watu wanazunguka kusema kwamba hujafanya kazi?” Kanze Dena alisema.

State House, KWA HISANI
State House, KWA HISANI
Image: Kanze Dena
State House, KWA HISANI
State House, KWA HISANI
Image: Kanze Dena

Msemaji wa ikulu, Kanze Dena amemtetea utendakazi wa rais Uhuru Kenyatta akisema kwamba sehemu alizofeli zilikuwa nje ya uwezo wake.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha habari nchi siku ya Ijumaa, Dena alitaja mpango wa ajenda nne kuu kama moja kati ya miradi mizuri kutoka kwa serikali ya Kenytta na kwamba wakenya sasa wanaweza kupata nyumba kwa bei nafuu, uwepo wa chakula, uzalishaji na afya bora kwa asilimia kubwa ya wakenya.

“Rais amefanya kazi kubwa huku akiwaweka wakenya mbele,” Dena alisema.

Aidha amesema kwa rais hawezi kulaumiwa kwa ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana akisema kwamba hiyo ni changamoto inayoyakumba mataifa mengi duniani.

“Bei za vyakula zimepanda kutokana na mfumukobei ulioletwa na janga la Corona. Taifa letu linakua na idadi ya watu inazidi kuongezeka kila ucho na hivyo basi hatruwezi kukidhi mahitaji yao kwa awamu moja,” msemaji huyo alikiri.

Kanze Dena aliongezea kwamba Kenyatta amepiga hatua kubwa katika kumaliza ufisadi nchini kutokana na idadi kubwa ya wafanyikazi wa umma ambao wamefikishwa mahakamani na kuhukumiwa.

“Ni suala linaloendelea, sio jambo linaloweza kuafikiwa kizembezembe. Kwa mfano kama KPLC, watu wameachishwa kazi, KEPSA watu waliondolewa ofisini,”Kanze alielezea.

Alimtetea Kenyatta kutokana na handshake aliyoifanya na Raila Odinga, akisema kwamba naibu rais alifahamishwa kila kitu bila kutengwa, na mchkato huo ulilenga kuleta amani miongoni mwa wakenya.

Aliongezea kwamba wakati mwingine rais Kenyatta anaonyesha kugadhabisha kwake hadharani kutokana na viongozi wanaomuunga mkono Ruto kusema kwamba hajafanya maendeleo yoyote .

“Rais ni binadamu tu, wewe utahisi vipi wakati umefanya kazi na watu wanazunguka kusema kwamba hujafanya kazi?” Kanze Dena alisema.