Afisa wa polisi,mkewe na mtoto wateketea kwa moto Bomet

Muhtasari
  • Afisa wa polisi,mkewe na mtoto wateketea kwa moto Bomet
crime scene 1
crime scene 1
Image: HISANI

Afisa wa polisi, mkewe na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka minne waliteketea Jumamosi katika kisa cha moto ambao uliteketeza nyumba hiyo walipokuwa wamelala katika nyumba yao ya Kesebek huko. Longisa huko Bomet mashariki.

Tukio hilo ambalo lilikitikisa kijiji hicho kwa mshtuko na majonzi inasemekana limetokea majira ya saa mbili asubuhi huku chanzo cha moto huo kuteketeza kabisa nyumba hiyo yenye muundo wa mbao bado hakijafahamika.

Akithibitisha kisa hicho, chifu wa Longisa Paul Langat alisema juhudi za majirani walioitikia wito wa kuzima moto huo hazikufua dafu kwani tayari moto huo ulikuwa umeteketeza nyumba nzima.

Binti mkubwa ambaye alikuwa katika nyumba tofauti alisema alimsikia babake akiomba msaada na kumfanya apige kelele jambo ambalo liliwavutia wakazi.

Ingawa haijulikani ikiwa kulikuwa na ugomvi wowote wa kinyumbani kati ya mume na mke, Langat alisema askari huyo alikuwa yupo Nairobi na alikuwa amefika tu nyumbani jioni kabla ya moto kuanza.

"Hatutaki kukisia kwa sasa kile ambacho kinaweza kuwa kimeanzisha moto huo lakini tunajua kwa sasa ni kwamba afisa huyo yuko Bungoma na amekuwa yupo Nairobi,” chifu alisema.

Aliongeza kuwa maafisa kutoka kampuni ya umeme ya Kenya pia wametembelea nyumba hiyo ili kuangalia kama kunaweza kuwa na tatizo la kuunganisha umeme.

Alisema maafisa wa usalama wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Miili ya marehemu ilihamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Longisa.