Muhtasari
•Asilimia 20 wanaamini kuwa hakutakuwa na wizi wa kura ilhali asilimia 10 hawana uhakika.
Wakenya wengi wanaamini kuwa uchaguzi wa urais wa Agosti 9 utakuwa huru na wa haki, utafiti wa TIFA unasema.
Utafiti huo unasema asilimia 37 ya Wakenya wana uhakika kuwa kutakuwa na uwazi katika uchaguzi wa mwaka huu.
Haya ni licha ya naibu Rais William Ruto ambaye ni mmoja wa wanaowania kiti cha urais kusema kuna uwezekano wa kura hizo kuibiwa.
Utafiti huo hata hivyo ulibainisha kuwa asilimia 32 ya Wakenya wanaamini kwa kiasi fulani kuwa uchaguzi huo utaibiwa.
Asilimia 20 wanaamini kuwa hakutakuwa na wizi wa kura ilhali asilimia 10 hawana uhakika.