Nilikuwa nasubiri Raila na Wanjigi nilipokamatwa-Miguna

Wakili huyo alizungumza Ijumaa alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Magina, eneo la Nyando, Kaunti ya Kisumu.

Muhtasari
  • Alisema ni watatu tu ndio wanajua walichopanga kufanya siku hiyo. Watatu hao walikuwa wamepanga kukutana saa nane kamili
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Image: Andrew Kasuku

Wakili Miguna Miguna amefichua kwamba alipokamatwa 2018, alikuwa nyumbani kwake Runda akiwasubiri Raila Odinga na mshirika wake wakati huo Jimi Wanjigi.

Alisema ni watatu tu ndio wanajua walichopanga kufanya siku hiyo. Watatu hao walikuwa wamepanga kukutana saa nane kamili.

"Siku nilipokamatwa kutoka nyumbani kwangu, nilikuwa nikisubiri Raila aje lakini badala yake polisi walikuja. Nilikuwa nikimsubiri yeye na Wanjigi, wanajua tulichokuwa tumepanga kufanya," Miguna alisema.

Wakili huyo alizungumza Ijumaa alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Magina, eneo la Nyando, Kaunti ya Kisumu.

Kukamatwa kwa Miguna mnamo 2018 kufuatia kuapishwa  kwa Raila Odinga katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi, ambapo aliapisha.

Miguna alifurushwa nchin tangu wakati huo, na kurejea nchini 20 Oktoba 2022.