'Lazima masuala ya wananchi yatangulie,'Ruto kwa Wabunge

Aidha aliwataka wabunge kuacha kujihusisha na masuala madogo kama vile mapitio ya Katiba ili kubadilisha ukomo wa muhula wa urais.

Muhtasari
  • Akizungumza Jumatano wakati wa mkutano wa Kikundi cha Wabunge wa Kenya Kwanza katika Ikulu, Ruto aliwaambia watekeleze majukumu yao ya ubunge kwa umakini
RAIS WILLIAM RUTO
Image: PCS

Rais William Ruto amewataka Wabunge kutanguliza miradi ambayo ina athari ya moja kwa moja kwa maisha ya Wakenya.

Akizungumza Jumatano wakati wa mkutano wa Kikundi cha Wabunge wa Kenya Kwanza katika Ikulu, Ruto aliwaambia watekeleze majukumu yao ya ubunge kwa umakini.

“Ulichaguliwa kuwatumikia watu; masuala yao lazima yatangulie,” alisema.

Aidha aliwataka wabunge kuacha kujihusisha na masuala madogo kama vile mapitio ya Katiba ili kubadilisha ukomo wa muhula wa urais.

"Kama Rais, sitashiriki katika juhudi zinazolenga kuvunja Katiba kwa maslahi ya kishenzi, ya ubinafsi na ya kibinafsi," alisema.

Ruto aliwaambia wabunge hao kuwasilisha na kupitisha kanuni zitakazorahisisha utekelezaji wa Hazina ya Hustlers.

Rais William Ruto amewaambia wabunge wa UDA kuwa hana nia ya kubadilisha katiba ili kuondoa  mihula ya rais.

Akizungumza Jumatano, Rais alisema wabunge hao wanapaswa kutanguliza miswada ambayo itaboresha maisha ya Wakenya.

Siku chache zilizopita, mbunge wa Fafi Salah Yakub aligonga vichwa vya habari baada ya kutoa matamshi ya kutaka kuondolewa kwa mihula ya rais.

Yakub katika pendekezo lake alisema umri ndio unapaswa kuzingatiwa umri na sio huduma ya muda.

Mbunge huyo wa UDA alidai kuwa baadhi ya wabunge wenzake tayari wanafanyia kazi muswada wa marekebisho ya Katiba ili kubadilisha mihula miwili rais na kuweka kizuizi kuwa umri wa miaka 75.