Mtahiniwa wa KCPE ajifungua mtoto wakati wa mitihani

Msichana huyo alijifungua kabla ya mtihani wa Hisabati kuanza.

Muhtasari

•Msichana huyo alifanya mtihani wake katika hospitali ya Marimanti

• "Hakutakuwa na udanganyifu katika mtihani huu," alisema Machogu.

Mtahiniwa mjamzito
Mtahiniwa mjamzito
Image: Maktaba

Huku wanafunzi wa darasa la 6 na  darasa la 8 wakianza mitihani wao wa kitaifa Jumatatu asubuhi, mtahiniwa mmoja wa KCPE alijifungua mtoto katika eneo la Tharaka, kaunti ya Tharaka Nithi.

Mtahiniwa huyo alijaliwa na baraka ya mtoto katika hospitali ya  Marimanti iliyo  eneo hilo kabla ya mtihani wa hisabati kuanza.

Mkurungezi wa elimu wa eneo hilo Bwana Solencio Maringe alisema kuwa mtahiniwa huyo anaendela kufanya mtihani wake huko hospitalini licha ya kujifungua.

Mbali na hayo waziri wa elimu Bwana Ezekiel Mchogu akizungumza wakati wa ufunguzi wa kontena la kwanza la mtihani mjini Mombasa alisisitiza kuwa usalama wa mtihani huo imeimarishwa.

"Hakutakuwa na udanganyifu katika mtihani huu," alisema Machogu.

Aliongeza kuwa helikopta zitasaidia kusambaza mitihani hiyo kutoka katika vituo 493 kote nchini.

Jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kwa mitihani hiyo mitatu ni 3,416,048.

Kati yao, watahiniwa 1,287,597 walisajiliwa kwa KPSEA, 1,244,188 kwa KCPE na 884,263 kwa KCSE.

Watahiniwa wa kidato cha nne watakalia mtihani wao Ijumaa ya Desemba 2 hadi Desemba 24 2022.