(Video) Polisi anaswa na CCTV akipekua mikoba ya wasimamizi wa mitihani ya KCPE

Afisa alikalia sofa na kuaza kuzipora pesa alizoziweka kwenye mfuko wake wa kaptura na kuondoka taratibu

Muhtasari

• Mtihani ulipokamilika walimu walalamikia pesa zao zilizokuwa zimechukuliwa.

• Polisi walionekana kutochukua hatua yoyote pindi tu taarifa hiyo iliripotiwa.

Wakenya mitandaoni wameghabishwa na afisa wa polisi aliyenaswa kwenye kanda ya CCTV akiiba pesa kutoka kwa wasimamizi wa mitihani ya kitaifa katika shule ya upili ya Kimulot iliyoko eneo bunge la Konoin, Kaunti ya Bomet.

Video iliyosaambaa kwenye mitandani ya kijamii tangu siku ya Jumatatu, inamwonesha afisa huyo wa polisi ambaye alikuwa ametumwa kuweka ulinzi wa mtihani wa KCPE kwenye shule hiyo akiingia katika darasa ambako mikoba ya walimu ilikuwa imewekwa. 

Afisa huyo ambaye yuko mbioni na aliyekuwa amevalia sare rasmi za polisi alikuwa ameshika  bunduki aina ya AK-47 mkononi. Alikalia kiti cha sofa kilichokuwa kimewekwa mikoba hiyo na kuanza kuchakura akitia vilivyomo mfukoni mwake.

Kamanda wa polisi alisema Mathews Mangira, mmoja wa mwalimu mmoja alilalamikia kupoteza  shilingi 100, mwingine alipoteza 900 na wengine watatu walipoteza 300.

Baada ya mtihani huo kukamilika, walimu walilalamikia kuwa pesa zao zilipotea kwa njia tata.

Kisa hicho cha aibu kiliripotiwa kwa maafisa hao lakini walidinda kutilia umakini licha ya malalamiko kutoka kwa wasimamizi wa mitihani.

Ingawaje kiwango cha fedha zilichoibwa hakikubainika, polisi walianzisha uchunguzi mara moja ili kubaini nani aliyekuwa nyuma ya kitendo hicho. Uchunguzi ulipelekea kamera za CCTV kupekuliwa ili kutoa ukweli.

Afisa wa polisi wa eneo hilo la Bomet ambaye alinukuliwa na jarida la Nation alisema 'Tumetuma maafisa katika eneo hilo ili kuthibitisha habari ya afisa inayoenea na kuchunguza iwapo habari hizo ni za ukweli ama la ili hatua zinazofaa kuchukuliwa zichukuliwe.''