Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Machakos aliyepigwa risasi na polisi afariki

Mwanafunzi huyo pamoja na wenzake walikuwa wakifanya maandamano dhidi ya kudorora kwa usalama katika eneo hilo.

Muhtasari

• Afisa wa polisi aliyempiga risasi alikamatwa na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Machakos.

Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Machakos auawa
Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Machakos auawa
Image: DCI

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Machakos aliyepigwa risasi na afisa wa polisi wakati wa maandamano ya wanafunzi Jumatatu amefariki. 

Mwanafunzi huyo alifariki katika hospitali ya Machakos Level 5 alikokuwa akipokea matibabu Jumatano asubuhi. 

Taarifa za kifo chake zilipokelewa na wengi wakiwemo wanafunzi wenzake kwa mshtuko. 

Alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia tukio hilo. 

Mwanafunzi huyo pamoja na wenzake walikuwa wakifanya maandamano dhidi ya kudorora kwa usalama katika eneo hilo. 

Afisa wa polisi aliyempiga risasi alikamatwa na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Machakos. 

Kulingana na idara ya DCI, Jumla ya bunduki 9 - bastola 5, tatu za G-3 na moja aina ya AK-47 zilichukuliwa kutoka kwa maafisa tofauti wa polisi. 

Silaha hizo zitafanyiwa uchunguzi katika Maabara ya Kitaifa ya Kitaifa ya DCI, ili kubaini kisayansi ni bunduki zipi zilitumika vibaya wakati wa maandamano.