Machakos: Polisi akamatwa kwa kumpiga mwanafunzi wa chuo risasi

Mwanafuzi huyo alipigwa risasi akiwa kwenye maandamano ya kukomesha ukosefu wa usalama ambao umekithiri mtaa huo.

Muhtasari

• Koplo Michael Mulwa anadaiwa kumpiga risasi mwanafunzi wa chuo kikuu cha Machakos Brilliant Anusu walipokuwa wakiandamana.

Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Machakos auawa
Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Machakos auawa
Image: DCI
Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Machakos auawa
Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Machakos auawa
Image: DCI

Afisa wa polisi anazuwiliwa katika kituo cha polisi cha Machakos kwa makosa ya kumpiga risasi na kumjeruhi vibaya mwanafunzi wa chuo kikuu.

Afisa huyo, Koplo Michael Mulwa, alidaiwa kumpiga risasi mwanafunzi wa chuo kikuu cha Machakos Brilliant Anusu.

Ripoti ya DCI ilisema mwanafunzi huyo alikuwa anaandamano na wenzake kutokana na kuzorota kwa usalama katika eneo hilo.

Anusu ambaye amelazwa katika hospitali ya  Machakos katika hali mbaya, alikuwa na wenzake waliokuwa wakikabiliana na maafisa wa polisi siku ya Jumatatu 5, 2022.

Idara ya DCI ilinasa bunduki na silaha zingie kwa maafisa hao ambazo zinaendelea kufanyiwa uchunguzi na kitengo hicho cha upelelezi ili kubainisha kisayansi silaha hizo ni zipi zilitumika kutekeleza unyama huo.

''Jumla ya bunduki 9 zikiwemo bastola 5, G-3 tatu na bunduki moja aina ya AK-47 pia zimenaswa kutoka kwa maafisa tofauti wa polisi na zitafanyiwa uchunguzi'' ripoti ya DCI ilisoma.

Tukio hili linajiri baada ya maafisa wengine wawili katika eneo hilo kukamatwa kwa madai ya kumuibia mwanafunzi wa chuo kikuu cha Machakos simu na vitu vingine vya thamani.

Kevin Sila na David Muringu ambao wako korokoroni wanaaminika kutumia mabavu kutekeleza wizi huo.

Wanafunzi hao walikuwa wanaelekea kwenye chumba chao cha kukodi walipovamiwa na maafisa wa usalama.

Waliokolewa na wanafunzi wenzao ambao walisikia mayowe.

Raia ambao walikuwa wamepandwa na mori, waliwapigia polisi cha Machakos ambao waliwakamata maafisa hao na kuwafungulia mashtaka ya wizi.