Molo: DCI wanamsaka mwanamume aliyemuua mpenzi wake na kutoroka

DCI walipata kisu cha mboga kikiwa na damu kwenye tukio

Muhtasari

• Polisi bado hawajabainisha kilichosababisha mwanaume huyo kufanay tukio hilo la ajabu.

• Jamaa huyo alitoroka baada ya kutekeleza unyama huo.

• Mwili wa mwanadada huyo ulipatwa umegubikwa kwenye sofa ndani ya nyumba hiyo.

Mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu
Image: Instagram//Azam

DCI huko Moro, Kunti ya Nakuru wameanzisha msako mkali wa kumtafuta mwanamume ambaye yuko mbioni baada ya kumuua mpenzi wake.

Mwanamume huyo, Moses Njeri anaripotiwa kumdunga mpenzi wake Hannah Ndirangu mwenye umri wa miaka 28  kwa kisu kwenye kifua kabla ya kutoroka kufuatia mgogoro ambao haujabainika halisi.

Mwanamke mmoja aliyekuwa jirani alikuwa wa kwanza kupata mwili wa mwanadada huyo baada ya kupata mpenyo kwenye nyumba hiyo ya mbao alilotumia mshukiwa huyo kutorokoea.

Hali ya sintofahamu ilianza kujiri baada ya wanakijiji kugundua tukio hilo la kinyama walipouona mwili huo wa mwanadada wa makamo umetandazwa kwenye sofa.

Maafisa wa upelelezi wa DCI, walifika kwa kasi kama umeme walipojulishwa tukio hilo na kupata kisu cha kukatia mboga kilichokuwa na damu na kilichotumika kama zana ya mauaji.

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi hospitali ya kaunti ya Molo huku kikosi cha DCI kikiahidi kutolaza damu hadi mshukiwa huyo wa mauaji atakapokamatwa.

Haya yanajiri baada ya tukio lingine la kuhuzunisha kutokea eneo la Ongata Rongai ambapo mwanadada mmoja alishikwa kwa madai ya kumuua mpenzi wake.

Kulingana na ripoti ya DCI, mwanadada huyo Jacklyn Zakayo mwenye umri wa miaka 27, alikatisha maisha ya jamaa wake Kennedy Bitonye Oyatsi aliyekuwa na umri wa miaka 47,  kwa kile kilichojulikana kuwa mzozo wa kinyumbani.