Washukiwa wa wizi wa vyuma vya reli wasakwa Nakuru

Washukiwa walitoroka walipowaona maafisa wa polisi waliokuwa wanashika doria.

Muhtasari

• DCI wameanzisha msako mkali wa kuwatafuta washukiwa waliokuwa wakijaribu kuiba vyuma vya reli katika eneo la Rongai, kaunti ya  Nakuru.

Pingu
Image: Radio Jambo

Maafisa kutoka kitengo cha DCI wameanzisha msako mkali wa kuwatafuta washukiwa waliokuwa wakijaribu kuiba vyuma vya reli katika eneo la Rongai, kaunti ya  Nakuru.

Kulingana na ripoti ya DCI, washukiw hao walikuwa wanatekeleza uhalifu huo majira ya usiku, tayari walikuwa wameng'oa zaidi ya vyuma 150 na  kuzipakia kwenye lori lilokuwa limeengeshwa kando mwa reli walipoonekana na maafisa wa polisi.

Washukiwa walitoroka pindi tu walipowaona polisi hao ambao walikuwa wanapiga doria katika eneo hilo mwendo wa saa sita usikuu wa Jumatatu.

''Polisi walipofika, wahalifu hao walitoroka na kuacha lori lenye namba ya usajiri  KCH 646T iliwa imesheheni vyuma hivyo vilivyoharibiwa. Zilikuwa zimengolewa kutoka kwa laini inayoanzia Rongai hadi kampi ya Moto na Solai.'' DCI ilisema.

Mwaka jana, serikali ilipiga marufukua biashara ya vyuma kuu kuu kufuatia uharibifu wa mali ya umma ambao umekithiri.

''Uhalibifu wa miundo mbinu ni kosa kubwa. Watakaokamatwa watakabiliwa na mashataka ya kuhujumu uchumi na ugaidi.'' taarifa ya DCI ilisomeka.