Kenya imepoteza mwanajamii mashuhuri-Raila asema huku akimuomboleza Ker Willis

Waziri Mkuu huyo wa zamani aliongeza kuwa pia ni hasara kubwa kwa Kenya kama nchi.

Muhtasari
  • Alieleza Otondi kama mwanajamii mashuhuri, huku akiwapa rambirambi familia yake na marafiki
Ker Willis Otondi
Image: KWA HISANI

Kiongozi wa ODM Raila Odinga ameomboleza kifo cha mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Waluo Ker Willis Otondi.

Alikufa akiwa na umri wa miaka 98.

Katika taarifa yake Ijumaa, Raila alisema kuaga kwa Ker Otondi ni hasara kubwa kwa jamii ya Waluo.

Waziri Mkuu huyo wa zamani aliongeza kuwa pia ni hasara kubwa kwa Kenya kama nchi.

Alieleza Otondi kama mwanajamii mashuhuri, huku akiwapa rambirambi familia yake na marafiki.

"Kuaga kwa Ker Willis Otondi kumetuacha na moyo mzito; ni hasara kubwa kwa taifa zima la Waluo. Kenya imepoteza mwanajamii mashuhuri," Raila alisema.

"Nina huzuni kwa taifa la Wajaluo kumpoteza kwa wakati huu. Rambirambi zangu zinaenda kwa familia yake, marafiki, na jamii nzima."

Otondi alikata roho katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga alikokuwa amelazwa kwa muda.