Mhubiri Pius Muiru amtetea vikali mhubiri Ezekiel Odero

“Acheni kumhusisha Ezekiel na uhalifu dhidi ya binadamu, inaonekana kanisa liko kwenye majaribio,” alisema.

Muhtasari

• Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai aliwasilisha hati ya kiapo akiomba mahakama imnyime Odero dhamana kwa sababu uhalifu unaochunguzwa ni mzito.

Mhubiri Pius Muiru
Mhubiri Pius Muiru

Mwinjilisti Mchungaji Pius Muiru amemtetea kasisi Ezekiel Odero.

Akiwahutubia wanahabari, Muiru alidai kuwa Ezekiel anahusishwa na uhalifu dhidi ya ubinadamu, utekaji nyara na ulaghai lakini wenzake wanatumai wanataka madai hayo kushughulikiwa kwa njia ya haki.

“Acheni kumhusisha Ezekiel na uhalifu dhidi ya binadamu, inaonekana kanisa liko kwenye majaribio,” alisema.

"Tuna watu wengi sana ambao wanakubaliana na Mchungaji Ezekiel, hali ni kwamba wengi wanasubiri kuona jinsi hukumu hiyo itatolewa."

Muiru pia alisema yanayomkabili Ezekiel ni jambo la kawaida ambalo watu wanalijua, akiongeza kuwa viongozi wa kanisa hilo hawapingani na uchunguzi wowote.

"Kitu pekee tunachopinga ni mateso ya kimyakimya na mateso ambapo mtu anajaribu kumhusisha mchungaji Ezekiel na uhalifu."

Siku ya Jumanne, mahakama iliamua kwamba Ezekiel atakaa kwa siku mbili zaidi chini ya ulinzi wa polisi akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake Mei 4.

Wiki iliyopita Ezekiel alifikishwa katika Mahakama ya Shanzu baada ya kudaiwa kutenda kosa la mauaji, kufanikisha watu kujitoa uhai, utekaji nyara, itikadi kali, mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili dhidi ya watoto, ulanguzi wa fedha.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai aliwasilisha hati ya kiapo akiomba mahakama imnyime Odero dhamana kwa sababu uhalifu unaochunguzwa ni mzito.

Mawakili wake wanasisitiza kuwa hana hatia na wanataka aachiliwe.

Ezekiel na Muiru, walikutana miaka ya 2000. Hii ni baada ya kujiunga na Kanisa la Maximum Miracle lake Muiru akiwa mwalimu wa kwaya na baadaye mwalimu wa nyimbo za kusifu na kuabudu.

Kulingana na idara zinazochunguza suala hilo, kukutana kwake na Muiru kulibadilisha maisha yake pakubwa na kulichangia yeye kuanzisha kanisa lake huku akidumisha uhusiano wa karibu na Muiru.