Passaris: Kwa nini sitajiunga na maandamano ya Azimio ikiwa yatarejea

Raila alisitisha mazungumzo hayo akisema kambi ya Kenya Kwanza ilishindwa kuzingatia matakwa yao.

Muhtasari
  • Akizungumza Jumanne, mbunge huyo alisema hatajiunga na maandamano kwa sababu ya matatizo ya kiafya.
Mwakilishi wa kike Nairobi, Esther Passaris.
Mwakilishi wa kike Nairobi, Esther Passaris.
Image: Facebook

Mwakilishi wa Wanawake wa Nairobi Esther Passaris ana sababu za kina kwa nini hatajiunga na maandamano ya Azimio siku zijazo.

Akizungumza Jumanne, mbunge huyo alisema hatajiunga na maandamano kwa sababu ya matatizo ya kiafya.

Mwakilishi wa wanawake wa Nairobi alisema anaamini watu wana haki ya kuandamana.

"Ninasumbuliwa na msongo wa mawazo baada ya kiwewe tangu 2017, sijawahi kupona na inazidi kuwa mbaya. Sitajiunga na maandamano. Naamini kila mtu ana haki ya kuandamana lakini kwa sababu za kiafya, siendi kwa maandamano," Passaris amesema.

Alisema kuwa upinzani na serikali wanaweza kuketi na kuzungumza ili kuboresha maisha ya Wakenya.

"Tuna watu wakali kutoka pande zote mbili. Wanasema kuwa hawataki hendisheki lakini Baba (kiongozi wa Azimio Raila Odinga) anataka nchi itawaliwe vyema," alisema.

Passaris alisema gharama ya juu ya maisha itapanda kabla haijashuka.

Haya yanajiri baada ya kiongozi wa Azimio Raila Odinga kusitisha mazungumzo ya pande mbili na kutishia kuitisha demos iwapo masuala hayatashughulikiwa.

Raila alisitisha mazungumzo hayo akisema kambi ya Kenya Kwanza ilishindwa kuzingatia matakwa yao.

Bosi huyo wa upinzani amekuwa akiongoza msururu wa mademu kote nchini kupinga gharama ya juu ya maisha miongoni mwa masuala mengine.

Hata hivyo kiongozi wa Azimio hajatangaza maandamano yatarejea siku gani.