Wakenya wenye tattoo wafungiwa nje katika usajili wa kujiunga na Huduma ya Kitaifa ya Vijana

Baadhi ya vijana walioondolewa walihoji uamuzi wa kuwafungia nje ya zoezi hilo kwa sababu tu ya usanii wao.

Muhtasari

• Mamlaka haikutoa sababu mara moja ya hatua hiyo lakini waliahidi kutoa taarifa mwishoni mwa zoezi hilo, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Baadhi ya vijana hao walihoji uamuzi wa kuwafungia nje ya zoezi hilo kwa sababu tu ya sanaa yao ya mwili
Baadhi ya vijana hao walihoji uamuzi wa kuwafungia nje ya zoezi hilo kwa sababu tu ya sanaa yao ya mwili
Image: BBC

Vijana kadhaa wa Kenya wamefungiwa nje ya usajili unaoendelea katika shirika la vijana la serikali kwa kuchora tattoo kwenye miili yao.

Ingawa walitimiza sifa za kitaaluma na pia kufaulu mtihani wa utimamu wa mwili ili kujiunga na Huduma ya Kitaifa ya Vijana (NYS), walionekana kutostahiki kwa sababu ya kuchora tattoo.

Baadhi ya vijana walioondolewa walihoji uamuzi wa kuwafungia nje ya zoezi hilo kwa sababu tu ya usanii wao na kuzitaka mamlaka hizo kuangalia upya hatua hiyo.

Mamlaka haikutoa sababu mara moja ya hatua hiyo lakini waliahidi kutoa taarifa mwishoni mwa zoezi hilo, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Shughuli ya uajiri wa NYS, ambayo inafanyika kote nchini, ilianza Jumatatu, na inatafuta kuajiri angalau vijana 15,000.