Obinna afichua anayemsapoti kati ya Mulamwah na Sonie kuhusu zogo la malezi ya mtoto

“Huwezi jua ama ni Mulwamwa au ni Sonie. Wakati mwingine sehemu inayoongea zaidi ni ile inayoaminika au inayocheza zaidi au ile ambayo haisemi au kusema kwanza," Obinna alisema.

Image: MAKTABA

Huku zogo la mchekeshaji Mulamwah na babymama wake Carrol Sonie likiendelea kuchukua mkondo tofauti usiotatajiwa, Wakenya mbali mbali wamejitokeza katika mitandao ya kijamii kuonesha ni nani wanayesimama naye baina ya wapenzi hao wa zamani.

Mchekeshaji Oga Obinna ni mmoja wa watu ambao wamejitoma mazima katika zogo hilo na kuonyesha ni nani ambaye wanasimama naye katika kesi hiyo ambayo tayari Mulamwah amedokeza kuwa itaishia mahakamani katika juhudi zake za kutaka kupata nafasi ya kumuona binti yake Keilah Oyando.

Kupitia video ambayo alipakia kwenye insta story yake, Obinna alisema kwamba licha ya watu wengi kusimama na kila mmoja, lakini kuna mambo mengi ambayo yanaendelea baina ya wawili hao ambayo hajaonekani hadharani.

"Huu ni mtazamo wangu juu ya hali nzima. Wakati mwanamume na mwanamke na mtoto mchanga wanahusika, kwa kawaida kuna mambo mengi ambayo watu wa nje hawayajui, ambayo ni wawili tu wanajua na kuna sehemu moja ambayo kwa kawaida haifai kwa sehemu nyingine.”

“Huwezi jua ama ni Mulwamwa au ni Sonie. Wakati mwingine sehemu inayoongea zaidi ni ile inayoaminika au inayocheza zaidi au ile ambayo haisemi au kusema kwanza, haijalishi, kwa kawaida kuna mengi ambayo watu hawayajui.”

Kwa maana hiyo, Obinna alisema kwamba yeye anasimama upande wa mtoto, akisema kwamba inafaa mtoto aachwe ili kujionea kutoka pande zote mbili.

"Watu wanachukua upande wa Mulamwah, wengine wanachukua upande wa Sonie. Ninachukua upande wa mtoto, iweje turuhusu mtoto kuwaona wazazi wote wawili na kisha tusawazishe kutoka hapo, kupitia mahakama bila shaka kwa sababu tukimwachia mtu mmoja, mtu mmoja atataka kujipendelea. Ninachukua upande wa mtoto," alisema.

Mnamo Jumanne, Mulamwah alielezea nia ya kumshtaki Sonie kwa unyanyasaji wa watoto na kukashifu.

Katika notisi yake ya kesi ya sheria ya Februari 4, Mulamwah alimshutumu Sonnie kwa kumwita baba aliyekufa bado, alidai, yeye ndiye aliyefanya mzazi mwenzake kutowezekana. Pia ananuia kumshtaki Muthoni kwa sababu ya kubadilisha majina rasmi ya binti yao bila idhini yake.

Hii ilikuja muda mfupi baada ya wawili hao kurushiana vijembe kupitia challenge ya baby daddy na baby mama wa Kenya katika mitandao ya kijamii.

Sonie alifunguka kwamba alimwambia bintiye babake alifariki.