Mwanafunzi wa zamani wa JKUAT aliyetoweka Victor Kibet ampigia simu baba yake, asema yu hai

Mwanafunzi huyo wa zamani wa JKUAT aliripotiwa kutoweka mnamo Machi 18.

Muhtasari

•Baba yake Paul Mutai alisema alimpigia simu siku ya Ijumaa kumwambia yuko vizuri.

•Mutia, hata hivyo, hakufichua mengi kuhusu alikokuwa na yuko na nani.

Victor Kibet
Victor Kibet
Image: HISANI

Mwanafunzi wa zamani wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta Victor Kibet ambaye alitoweka mwezi uliopita yu hai.

Babake Paul Mutai alisema alimpigia simu siku ya Ijumaa kumwambia yuko vizuri.

Mutia, hata hivyo, hakufichua mengi kuhusu alikokuwa na yuko na nani.

Mwanafunzi huyo wa zamani wa JKUAT aliripotiwa kutoweka mnamo Machi 18.

Kibet mwenye umri wa miaka 23, anayesemekana kuishi maisha ya kifshsri kabla ya kutoweka, inadaiwa alikuwa akifurahia mchezo wa pool katika eneo la burudani katika kaunti ya Kiambu kabla ya kuripotiwa kukamatwa na watu waliodai kuwa maafisa wa polisi.

Walioshuhudia walidai kuwa walimwona akiwekwa ndani ya Subaru iliyokuwa ikimsubiri, ambayo iliondoka kwa kasi kutoka eneo la tukio, ikifuatiwa kwa karibu na gari aina ya double cab.

Tangu wakati huo, aliko Kibet lilikuwa limesalia kuwa kitendawili, huku polisi wakizidisha msako wa kumtafuta tajiri huyo kijana.

Kibet, ambaye mara nyingi alionekana kama kielelezo cha 'ndoto ya Kenya' ambayo vijana wengi na watu wa milenia wanatamani kutimiza, alikuwa na kipengele cha kushangaza kwenye hadithi yake - chanzo kisichojulikana cha utajiri wake ambacho kilizua mijadala kwenye mitandao ya kijamii.

Licha ya kutokuwa na kazi inayojulikana, Kibet aliripotiwa kumiliki magari ya hali ya juu zaidi.

Madai ya Kibet ya kumiliki magari mengi ya kifahari yalizua taharuki miongoni mwa wengi.

Kutekwa nyara kwake kunadaiwa kuhusishwa na msururu wa utapeli mtandaoni.

Ingawa haijafahamika nani alikuwa nyuma ya utekaji nyara huo, kulikuwa na maswali kuhusu utajiri wake na hasa chanzo.

Hata hivyo, siku chache baada ya kutoweka, babake alidai kuwa mtoto wake alitaja kuanzisha biashara na marafiki zake lakini hakutoa maelezo zaidi na kukashifu madai kwamba mwanawe alikuwa katika utapeli.