Uchunguzi waanzishwa huku mwanamke akiripotiwa kufariki akiavya mimba, Embakasi

Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana ukiwa umelala kitandani bila majeraha yoyote.

Muhtasari

• Maafisa wa upelelezi pia wanachunguza kisa ambapo mwili wa msichana wa umri wa miaka minane ulipatikana kwenye kitanda chake eneo la Ruai, Nairobi.

CRIME
Image: MAKTABA

Polisi wamesema wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja anadaiwa kufariki kutokana na jaribio la kuavya mimba eneo la Embakasi.

Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana ukiwa umelala kitandani bila majeraha yoyote.

Mwili wake ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti.

Maafisa wa upelelezi pia wanachunguza kisa ambapo mwili wa msichana wa umri wa miaka minane ulipatikana kwenye kitanda chake eneo la Ruai, Nairobi.

Mamake aliripoti kwa polisi kwamba kisa hicho kilitokea Jumamosi mchana.

Alisema alikuwa ameamka na kuanza kazi za nyumbani lakini aligundua saa kadhaa baadaye kwamba binti yake alikuwa amechukua muda mrefu sana kuamka.

Mama huyo alisema alienda chumbani kwake na kujaribu kumwamsha bila mafanikio. Mama huyo alisema mwili ulikuwa mgumu na baridi kupiga mayowe kuomba msaada.

Polisi walizuru eneo la tukio na kuuchukua mwili huo hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kusubiri uchunguzi.

Huku hayo yakijiri, mwanamume mmoja alifariki kwa kujitoa uhai baada ya kujinyonga ndani ya nyumba yake katika lokesheni ndogo ya Komenya, Kaunti ya Siaya. Marehemu, 46, alijinyonga kwa kutumia kipande cha nguo ndani ya chumba chake cha kulala, polisi walisema.