Watu kadhaa wanahofiwa kukwama kwenye jengo la ghorofa tano lililoporomoka Nyamira

Idadi ya watu waliokwama kwenye jengo hilo haikujulikana hadi wakati wa kwenda kwa vyombo vya habari.

Muhtasari

• Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea kwa sasa.

Watu kadhaa wanahofiwa kukwama katika jumba la orofa tano ambalo linadaiwa kuporomoka eneo la Gesima huko Nyamira.

Idadi ya watu waliokwama kwenye jengo hilo haikujulikana hadi wakati wa kwenda kwa vyombo vya habari.

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea kwa sasa.