Ruto aongoza hafla ya kuapishwa kwa majaji wa mahakama kuu

Majaji hao walikula kiapo cha afisi kilichosimamiwa na Msajili Mkuu wa Idara ya Mahakama Winfridah Mokaya.

Muhtasari

• Majaji hao walikula kiapo cha afisi kilichosimamiwa na Msajili Mkuu wa Idara ya Mahakama Winfridah Mokaya. 

Rais William Ruto aongoza kuapishwa kwa majaji wapya wa Mahakama kuu katika Ikulu ya Nairobi mnamo Mei 14, 2024. Picha: PCS
Rais William Ruto aongoza kuapishwa kwa majaji wapya wa Mahakama kuu katika Ikulu ya Nairobi mnamo Mei 14, 2024. Picha: PCS

Rais William Ruto siku ya Jumanne aliongoza hafla ya kuapishwa kwa majaji 20 wa Mahakama kuu katika Ikulu ya Nairobi. 

20 hao walipendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama kuteuliwa kuwa majaji wa Mahakama Kuu. 

Walioapishwa ni pamoja na Moses Ado Otieno, Alice Chepngetich Bett Soi, Benjamin Mwikya Musyoki, John Lolwatan Tamar, Francis Weche Andayi, Andrew Bahati Mwamuye, Julius Kipkosgei Ng'arng'ar, Wendy Kagendo Micheni na Emily Onyando Ominde. 

Majaji wakijiandaa kuapishwa
Majaji wakijiandaa kuapishwa
Image: Tume ya Utumishi wa Mahakama

Wengine ni Helene Rafaela Namisi, Alexander Muasya Muteti, Julius Mukut Nangea, Benjamin Kimani Njoroge, Caroline Jepyegen Kendagor, Stephen Nzisi Mbungi, Linus Poghon Kassan, Noel Onditi Adagi Inziani, Tabitha Ouya Wanyama, Rhoda Cherotich Rutto na Joe Omido Mkutu. 

Majaji hao walikula kiapo cha afisi kilichosimamiwa na Msajili Mkuu wa Idara ya Mahakama Winfridah Mokaya. 

Jaji Mkuu Martha Koome, naibu wake Philomena Mwilu na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei pia walikuwepo. 

Akiongea baada ya kuapishwa, Rais Ruto alihimiza ushirikiano kote serikalini katika utoaji wa huduma sawia huku wakidumisha uhuru wa kila idara.