Polisi wa kutuliza ghasia washika doria mjini Eldoret huku vijana wakikusanyika kwa maandamano

Makao makuu ya serikali ya kaunti ya Uasin Gishu ni miongoni mwa maeneo muhimu ambapo usalama umeimarishwa.

Muhtasari

Vijana wameanza kukusanyika katika maeneo mbalimbali na wamepanga kufanya maandamano katika makundi mbalimbali.

Polisi wanashika doria katika mitaa ya Eldoret kabla ya maandamano.
Polisi wanashika doria katika mitaa ya Eldoret kabla ya maandamano.
Image: MATHEWS NDANYI

Polisi wa kutuliza ghasia wameshika doria mjini Eldoret ambapo vijana wameanza kukusanyika kwa ajili ya maandamano ya dhidi ya Mswada wa Fedha.

Mamia ya maafisa wa polisi wametumwa mitaani kabla ya maandamano.

Vijana hao wameanza kukusanyika katika maeneo mbalimbali na wamepanga kufanya maandamano katika makundi mbalimbali.

"Ni haki yetu ya kikatiba kupiga kura kila tunapokuwa na sababu ya kufanya hivyo na sasa ni kuhusu mswada wa fedha". Alisema kiongozi wa vijana Ben Ruto.

Makao makuu ya serikali ya kaunti ya Uasin Gishu ni miongoni mwa maeneo muhimu ambapo usalama umeimarishwa.

Imetafsiriwa na Davis Ojiambo.