Waandamanaji kadhaa waliripotiwa kupigwa risasi nje ya Bunge

Kisa hicho kilitokea wakati waandamanaji hao wakijaribu kuingia katika Majengo ya Bunge siku ya Jumanne.

Muhtasari
  • Polisi walilazimika kufyatua risasi baada ya waandamanaji hao kuanza kuandamana kuelekea Bunge ambako wabunge walikuwa wakipiga kura kupitisha Mswada huo wenye utata.
Image: CYRUS OMBATI

Watu kadhaa wamepigwa risasi katika mzozo mkali kati ya maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia na waandamanaji waliokuwa wamefanya maandamano kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

Polisi walilazimika kufyatua risasi baada ya waandamanaji hao kuanza kuandamana kuelekea Bunge ambako wabunge walikuwa wakipiga kura kupitisha Mswada huo wenye utata.

Kisa hicho kilitokea wakati waandamanaji hao wakijaribu kuingia katika Majengo ya Bunge siku ya Jumanne.

Gari la polisi pia lilichomwa moto na waandamanaji wakati wa ghasia hizo.

Takriban waandamanaji watatu waliripotiwa kupigwa risasi nje ya Majengo ya Bunge huku kundi la watu wakipambana na polisi.

Kundi hilo lilikuwa likipinga Mswada wa Fedha. Takriban wengine wanne walijeruhiwa na kuchukuliwa na ambulensi, mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei alisema.

Watatu hao walipigwa risasi na kuuawa walipokuwa wakikaribia majengo ya bunge. Kundi jingine lilikuwa limeteremsha lango karibu na Seneti.

Lori la polisi liliteketezwa nje ya bunge. Wabunge walihamishwa huku kundi hilo likikabiliana na polisi. Machafuko yaliendelea saa 3 usiku.