Jengo la ghorofa nne laporomoka Kasarani, idadi isiyojulikana ya watu wanaswa ndani

Jengo la ghorofa nne lililoporomoka lilikuwa ni nyumba ya kupangisha.

Muhtasari

•Jumba moja liliporomoka katika eneo la Infinity eneo la Mwiki Estate, eneo la Kasarani jijini Nairobi Jumatano jioni.

Jengo laporomoka Kasarani
Jengo laporomoka Kasarani
Image: HISANI

Jumba moja liliporomoka katika eneo la Infinity eneo la Mwiki Estate, eneo la Kasarani jijini Nairobi Jumatano jioni.

Timu ya St John Ambulance imekimbia katika eneo la tukio katika juhudi za uokoaji. Hakuna waathiwa wowote ambao wameripotiwa kufikia sasa.

"Timu zetu za kukabiliana na dharura zikikimbilia eneo la tukio. Taarifa zaidi zitafuata hivi punde," St John Ambulance ilisema kupitia Twitter.

Jengo la ghorofa nne lililoporomoka lilikuwa ni nyumba ya kupangisha.

Polisi wamesema kuwa shughuli za uokoaji bado zinaendelea. Kikosi cha Kenya Red Cross pia kimeonekana katika eneo la tukio.

Mengine yanafuata...