Msimamizi wa Uchaguzi wa Embakasi East aliyetoweka apatikana amefariki huko Oloitoktok

Polisi waliotembelea eneo la tukio walisema marehemu alionekana kuteswa hadi kufa.

Muhtasari

•Mwili wake ulipatikana Jumatatu kwenye kichaka katika eneo la Mariko na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo.
•Polisi wanataka kuangalia mazungumzo ambayo msimamizi huyo alikuwa nayo na wagombeaji wowote au mawakala wao kabla ya uchaguzi.

Image: HISANI

Afisa wa uchaguzi wa Embakasi Mashariki aliyetoweka amepatikana amefariki. Daniel Mbolu Musyoka alitoweka mnamo Agosti 11.

Alikuwa katika kituo cha kujumlisha kura cha East African School of Aviation alipotoweka saa mwendo wa saa nne kasorobo asubuhi.

Ripoti ya kutoweka kwake ilikuwa imetolewa kwa polisi.

Mwili wake ulipatikana siku ya Jumatatu kwenye kichaka katika eneo la Mariko na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo.

Polisi waliotembelea eneo la tukio walisema marehemu alionekana kuteswa hadi kufa.

Familia ya marehemu na polisi kutoka Embakasi walitembelea chumba cha kuhifadhia maiti na kuutambua mwili huo. Nia ya mauaji na waliomuua Mbolu bado haijajulikana.

Kulikuwa na mipango ya ilikuwa kuhamisha mwili huo hadi Nairobi siku ya Jumanne.

Hapo awali, maafisa wa polisi walipata picha za CCTV zinazoonyesha matukio ya mwisho ya Musyoka.

Picha hizo zilikuwa zikichunguzwa na kitengo cha uhalifu wa mtandaoni na polisi walisisitiza kuwa Musyoka alikuwa salama ingawa alikokuwa ilibaki kitendawili.

Alipotoa tangazo la kutoweka kwa Musyoka, mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema walijaribu kumtafuta lakini hawakufanikiwa.

"Familia ya Musyoka na Tume wamekuwa wakijaribu kumfikia bila mafanikio. Ripoti ya mtu aliyepotea imetolewa katika kituo cha polisi cha Embakasi," Chebukati alisema Jumatatu akiongeza kuwa hajulikani aliko.

Aliongeza kuwa wafanyikazi wengine wengi wa tume wamenyanyaswa na kutishwa.

Mke wa marehemu, Tabitha Mbolu na bintiye Prudence Mbolu walikuwa na mazungumzo ya mwisho naye kwa simu kabla ya kutoweka.

Prudence alifichua kwa wanahabari kwamba wafanyakazi wenza wa mumewe katika IEBC walimpigia simu baada ya kukosa kumpata kwa simu.

Polisi kwa upande wao walisema walikuwa wakimtafuta bila mafanikio. Timu tofauti zilikuwa zimetumwa kuzunguka jiji na kutafuta njia tofauti katika nia ya kumtafuta afisa huyo aliyepotea ambaye hakuwa amelala kwa siku tatu baada ya mchakato wa kujumlisha kura kuanza.

Maafisa hao walipata picha za CCTV zinazoonyesha matukio ya mwisho ya Musyoka.Kanda hiyo inachunguzwa na kitengo cha uhalifu mtandao.

Afisa mkuu alisema wagombeaji wote katika kura zilizohitimishwa ni watu wa kuangaziwa katika kesi hiyo.

Wanataka kuangalia mazungumzo ambayo msimamizi huyo alikuwa nayo na wagombeaji wowote au mawakala wao kabla ya uchaguzi.

“Alizungumza na nani kabla na baada ya uchaguzi? Mbona, walikuwa na mazungumzo ya aina gani,” alisema afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Polisi walisema kumekuwa na madai kwa vyama mbalimbali na wanafungamana kuthibitisha hilo.

Madai hayo ni pamoja na yale kwamba huenda alitolewa nje na vyama ambavyo havikufurahishwa na jinsi alivyoshughulikia uchaguzi lakini alikuwa amefanya makubaliano ya awali.

Aliyekuwa Kamishna wa IEBC Roselyn Akombe alituma ujumbe wa mshikamano kwa familia ya marehemu.

Akombe alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumamosi asubuhi kuwa "alikuwa akiomba kwamba Daniel Musyoka yuko salama na aungane tena na familia yake."

Alisema anafahamu matatizo ambayo wafanyakazi wake wa zamani na wafanyakazi wenzake walikuwa wakikabiliana nayo wakati wa kujumlisha kura za urais.

"Naweka wafanyikazi wangu wa zamani na wafanyikazi wenzangu katika mawazo na sala zangu wakati wa nyakati hizi ngumu. Najua unapitia nini. Bora ujasiri, "alisema.

Akombe alikimbilia New York na kujiuzulu katika marudio ya uchaguzi wa Marudio ya Urais wa 2017, akisema alihisi hayuko salama, na kwamba hana uwezo wa kufanya uchaguzi wa kuaminika.

Kamishna huyo wa zamani mwezi uliopita alitumia ukurasa wake wa Twitter kumkumbuka marehemu mwenzake Chris Musando, ambaye aliuawa miaka mitano kabla ya uchaguzi.

Musando, ambaye aliwahi kuwa Meneja wa Teknolojia ya Habari wa tume ya uchaguzi, alitoweka Ijumaa, Julai 28, 2017, baadaye mwili wake ulipatikana kwenye kichaka cha Kikuyu, kando ya mabaki ya mwandamani wa kike aliyetambuliwa kama Carol Ngumbu.

"Miaka mitano tangu ukabidhiwe kwa wauaji wa kikatili ili kuzuia juhudi za kuleta uchaguzi wa kuaminika nchini Kenya. Ingawa wasaliti wako wametuzwa na uadilifu katika uchaguzi unasalia hatarini, haki itatendeka, haijalishi itachukua muda gani,” alisema Akombe.