Hekaya za Abunuasi! Oparanya atangaza kuwania urais 2022

Siku chache baada ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi kutoka Magharibi mwa Kenya kwenye boma la katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi nchini Francis Atwoli, gavana wa kakamega na ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Wycliffe Oparanya ametangaza azma yake ya kuwania urais mwaka 2022.

Oparanya anasema ametimu viwango vya kuwa kiongozi wa taiafa hili kwa sababu ameshikilia nyadhifa mbalimbali serikalini, jambo ambalo linamfanya kuwa na weledi wa kuwa rais.

Azimio la Oparanya linajiri wakati ambapo mshikemshike unajiri katika chama cha Ford Kenya huku baadhi ya viongozi wa chama hicho wakimtimua  chamani Moses Wetangula kama kiongozi wao.

Japo kwa upande wake Wetangula ametupilia mbali taarifa hizo na kumteua Chris Wamlwa kama katibu mkuu, wadhifa alikuwa anaushikilia Eseli Simiyu aliyetimuliwa chamani na Wetangula.