Huwezi mfananisha Diamond Platnumz na mpuuzi yeyote Tanzania, Babu Tale

Screenshot_from_2019_12_01_13_45_08__1575197145_73864
Screenshot_from_2019_12_01_13_45_08__1575197145_73864
Mmoja wa mameneja wa lebo ya WCB Babu Tale amesema kuwa hakuna anayeweza kufananisha na Diamond Platnumz.

Kauli ya Boss Tale imejiri baada ya Diamond Platnumz kujaza ukumbi mkubwa wa mashabiki 70,000 Siera Leone.

Mapokezi ya staa mkubwa Afrika Diamond Platnumz almaarufu Simba yamewafanya wengi kuajabia.

Katika mji mkuu wa nchi ya SieraLeone, mashabiki walionekana kujawa na furaha na nyemi usoni kwa kumuona staa huyu.

https://www.instagram.com/p/B5hSCVAhXZB/

Michambo ya Boss Tale inaonekana kulenga Ali Kiba na ambaye alikuwa katika tamasha tofauti mjini Tabora.

Kiba ameanzisha fiesta kibao kwa jina AliKiba Unforgettable Tour zinazolenga kuwakonga nafsi mashabiki wake wengi nchini humo.

"Mimi nikisemaga naonekana mswahili ila siachi kusema hatutaki mumfananishe  na mpuuzi yoyote. Hii ni Freetown Sierra Leone Muda wao saa hizi ndio kwanzaa saa tano uwanja umejaa wanamsubiria mtoto wa Tandale...," Tale alichapisha Insta

https://www.instagram.com/p/B5gfLGTBszi/

Meneja huyu wa Simba alionekana kulinganisha kati ya idadi ya watu waliojaza Fiesta ya Wasafi na ukumbi wa Tabora wa Ali Kiba,

"Kuna jamaa eti anasema ooh kwanza akajaze pale shamba la bibi (akimaanisha uwanja mdogo wa taifa) then ndio ajaze uko nje tuamini😂😂😂 aiitaji kuaminiwa na watu walioamua kuchukia,sasa kama amjui shamba la bibi panaingiza watu elfu16 na usiku wa wasafi festival watu tuliopata ni elfu24 na hapa toa walioingia bure na wengine walioingia kwa janja janja. Ugenini kuingiza watu elfu70 tena uwanjani haya endeleeni kutafuta msanii namba moja sisi tunaitangaza..." Alisema Boss Tale.