Kama Wataka Kumuoa Silphrosa Haya Ndiyo Masharti Unayopaswa Kutimiza

Katika kipindi cha 'Auntie Boss' muigizaji, Sandra Anyango Dacha almaarufu 'Silphrosa' anajulikana kama mjakazi wake Mayweather. Isitoshe anajulikana kama mama mlafi aliye na watoto saba.

Katika mahojiano yetu naye mwezi mmoja uliopita, Silphrosa aliwashangaza wengi alipofichua kuwa bado hajaolewa ila hana mpenzi na isitoshe hajazaliwa mtoto.

Haya yalibainika wakti tulipomhoji kuhusu mambo ambayo mashabiki wake hawajui kumhusu na alikuwa na haya yakusema.

"Kitu moja ambacho watu hawajui ni kuwa naweza nengua kiuno vizuri sana."Alisema.

Kingine ni kuwa kama Silphrosa katika kipindi cha 'Auntie Boss' watu huona nikiwa nimeolewa na watoto wengi, wacha niwashtue. Sina watoto na bado sijaolewa, kwa hivyo kama kuna mtu ambaye anaona nikama anawezana na hii lori, anawezza tuma application nitakubali. Aliongeza kabla ya kupeana mukhtasari wa vitu anavyo angalia kwa mwanaume.

Cha kwanza napenda mwanaume anayeamini mungu, mwanaume ambaye ana heshima kwa mwanamke kwani mapenzi huja ukiwa na heshima.

&t=19s