'Kifo cha babangu kiliniuma sana' Msanii Wyre afunguka

Msanii mashuhuri Wyre amesema kwamba kifo cha babake mzazi ndicho kitu kilicho muuma sana maishani kwani alikua mwandani wake.

Akiongea kwenye mahojiano na radio jambo Wyre alisema

wakati wa mwisho mimi kulia ni baada ya kumpoteza babangu.

Babake Wyre aliaga dunia mwaka wa elfu mbili kumi na tano (2015) kabla Wyre atoe album yake ya 'Wanilinda'.

Wyre aliweza kusema kwamba hakuweza kuupigia debe wimbo wake ilivyostahili kwani alikua bado anaomboleza.

Aliongeza kwamba kitu atakachomkumbuka babake nacho ni kwamba alikuwa anampa motisha wa kuendelea na muziki.

Wakati nilipojiingiza kwenye muziki, babangu aliniunga mkono na alifanya kila juhudi kuwa mwelekezi wangu.

Alitupa moyo kwa kutuhimiza tumwimbie tulipokuwa nyumbani.

Hivi majuzi Wyre alisema kwamba kuoa mke wake wa miaka kumi mara ya pili ni kwa sababu ndoa ni kitu anachokidhamini kwa dhati.

Nashukuru mungu sana ya kwamba nina ndoa imara.

Kitu ambacho kimefanya ndoa yangu isimame kwa miaka kumi ni kwamba mimi na mke wangu tuna ongelelea maswala kwenye ndoa muda tu yanapojitokeza.

Wyre ambaye ni baba wa mtoto mmoja alisema sababu kuu ya kuweka familia yake mbali na mitandao ya kijamii ni kwa sababu hataki wadhulumiwe kwa hali yoyote ile.