LUCKY ESCAPE:Kobe Bryant na Mkewe walikuwa na makubaliano ya kutosafiri ‘pamoja’  katika helikopta .

Kobe Bryant and wife
Kobe Bryant and wife
Nyota wa zamani wa NBA  aliyeaga dunia Kobe Bryant na mkewe  Vanessa walikuwa wamekubaliana kwamba hawatakuwa wakisafiri katika helikopta pamoja imedaiwa.

Kobe liaga dunia pamoja na bintiye mwenye umri wa miaka 13  Gianna na watu wengine wanane.

Kobe na mkewe wamekuwa katika ndoa tangu mwaka wa 2001  na kulingaa na jarida moja la  People mkewe hakupendelea kusafiri naye katika helikopta. Kobe mweye umri wa miaka 41  alikuwa tu akimtumia rubani mmoja Ara Zobayan  ambaye pia aliaga dunia katika ajali hiyo ya siku ya jumapili. Kobe awali amewahi kuzungumza kuhusu  mapenzi yake ya kutumia helikopta ili kuepuka msongamano wa magari alipokuwa akiichezea timu ya  Los Angeles Lakers.

Kobe alikuwa akielekea katika chuo chake cha mafunzo ya mchezo wa vikapu  cha  Mamba Sports Academy  kwa mchuano wa vijana  pamoja na  binti yake  Gianna,  alikuwa pia na mama na binti Sarah na Payton Chester,  kocha wa timu ya wasichana ya mchezo wa vikapu  Christina Mauser, kocha mmoja wa mchezo huo shuleni  John Altobelli  na mkewe  Keri  pamoja na binti yao  Alyssa, wakati ndege hiyo ya helikopta ilipoanguka katika milima Calabasas  iliyojaa ukungu . Amemwacha mkewe Vanessa mwenye umri wa miaka 37  na binti zao Natalia, 17, Bianka, 3,  na  Capri, aliyezaliwa Juni  2019.