Man City wakerwa na hatua ya Arsenal kumfuatilia Mikel Arteta

arteta (1)
arteta (1)
Manchester City wamekerwa na hatua ya Arsenali ya kumfuatilia kocha wao msaidizi Mikel Arteta na wameionya klabu hiyo kuwa itawabidi watoe donge nono ili wamnyakue kocha huyo.

Aidha, Arteta anatarajiwa kukutana na kiongozi mkuu wa Arsenal Josh Kroenke kwa ajili ya kufanya usajili wa tatu na wa mwisho huku akikaribia kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Unai Emery aliyetimuliwa mwezi uliopita.

Hata hivyo, Arteta yuko tayari kuacha wadhfa wake na kuchukua hatamu kama kocha wa Arsenali. Mzaliwa huyo wa Uhispaia ambaye hapo awali alichezea Arsenali alifanya mazungumzo na wasmamizi wa klabu hio ya London na inaaminika bado wanasubiri kumpiga msasa zaidi kabla ya kuteuliwa.

Kocha wa zamani wa Real Madrid, AC Milan  na Chelsea Carlo Ancelotti ameafikia makubaliano na klabu ya Everton ili kuchukua hatamu kama kocha mkuu.

Mazungumzo hayo yalifanyika jana baada ya Muitaliano huyo kuwasili Uingereza, siku kadhaa baada ya kufutwa kazi kama kocha wa Napoli.

Ancelotti amesalia na makubaliano ya sheria na masharti tu kabla ya kuchukua rasmi mahala pa Marco Silva ambaye alichujwa wiki mbili zilizopita.

Hata hivo kocha wa muda Duncan Fergusson atasalia kama msaidizi wake.

Wilfred Zaha alisawazishia Crystal Palace katika dakika ya 76 dhidi ya Brighton na kuhakikisha mechi hiyo ya ligi kuu Uingereza iliishia sare ya 1-1. Neal Maupay alikua ameweka Brighton kifua mbele katika kipindi cha pili ya mechi hio ya kusisimua.

Brighton wamesalia katia nafasi ya 13 kwenye jedwali huku Palace wakiwa katika nafasi ya tisa baada ya mechi 17.