Safaricom imemetaua Michael Joseph kuwa mwenyekiti mpya wa bodi yake . Anaichukua nafasi hiyo kutoka kwa Nicholas Ng’ang’a ambaye anastaafu baada ya kuiongoza bodi ya kampuni hiyo kwa miaka 16 .
Safaricom itatoa tangazo hilo rasmi kwa umma wakati wa mkutano wake wa kila mwaka siku ya alhamisi.
mwenyekiti wa bodi ana jukumu la kusimamia oparesheni na uongozi wa bodi ili kuunda ajenda ifaayo kwa ufanisi wa kampuni hiyo .
Michael Joseph ndiye afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo ,nafasiambayo aliishikilia kuanzia julai mwaka wa 2019 hadi machi mwaka wahuu . Alijiunga na kampuni hiyo septemba tarehe 8 mwaka wa 2008 .
Awali aliwahi kuwa afisa mkuu mtendani wa safaricom kuanzia julai mwaka wa 2000 wakati kampuni hiyo ilipozinduliwa upya kama biashara ya pamoja ya Vodafone UK na Telkom Kenya hadi alipostaafu novemba mwaka wa 2010.