Huenda ligi kuu ya Uingereza ikarejea tena Juni 8 mwaka huu

NA NICKSON TOSI

Ligi kuu ya Uingereza huenda ikarejelea mechi zake baada ya kamati simamizi ya ligi hiyo kuandaa kongamano na wasimamizi wa vilabu vyote vinavyoshiriki katika ligi hiyo kupitia njia ya video.Katika mazungumzo ,ili bainika kuwa huenda mechi zilizokuwa zimesalia ,kuchezwa bila ya mashabiki na baada ya serikali kutoa mwongozo mwafaka unaostahiki.

Shirikisho la soka la ulaya UEFA limekuwa likishinikiza kumalizwa kwa ligi zote ili kutoa nafasi ya kuandaa fainali ya kombe la mabingwa bara ulaya mnamo Agosti 29.

Timu za Uingereza zilikuwa zimesalia na mechi kati ya 9-10 na inadaiwa kuwa mechi zilizosalia huenda zikachezwa kwa majuma 5

Ligi kuu ya Uingereza ilisimamishwa baada ya baadhi ya makocha na wachezaji kupatikana na virusi vya Corona.