Rashford na Saka waondolewa kwenye kikosi cha Uingereza

saka
saka

Mchezaji wa Manchester United Marcus Rashford na winga wa Arsenal Bukayo Saka wameondolewa kwenye mechi zijazo za kufuzu Kombe la Dunia England dhidi ya Albania na Poland.

Rashford alijiunga na kikosi cha Gareth Southgate licha ya kuwa na jeraha la mguu na atarejea United baada ya tathmini zaidi.

Saka hakuwa amejiunga na kikundi kwa sababu ya jeraha la mguu. Southgate alikuwa na matumaini kuwa wawili hao watakua sawa kushiriki lakini imeamuliwa hawatakuwa sawa vya kutosha katika duru hii ya mechi za kimataifa.

England inasafiri kwenda Tirana kukabiliana na Albania katika mechi yao ya kufuzu ya Kundi I kesho kabla ya kuwakaribisha Poland huko Wembley Jumatano.

Kiungo wa kati-nyuma wa Southampton Jannik Vestergaard, 28, anasema kila mara imekuwa "jambo linalomtia moyo " kuhusishwa na klabu kubwa baada ya ripoti kwamba Tottenham wana nia ya kusaini mkataba na mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark 

Hali ya baadaye ya Mkufunzi Zinedine Zidane katika Real Madrid baada ya msimu uliosalia imesalia kutojulikana, huku shirikisho la soka la Ufaransa likionyesha kumtaka. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 48-bado ana mkataba na Real Madrid hadi mwaka 2022.

Mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez anaendelea kupata nafuu na  anaweza kushiriki kwa  Olimpiki msimu huu huko Tokyo, hii ni kulingana na meneja wa Mexico Gerardo Martino.

Jimenez hajacheza tangu alipopata jeraha la kichwa wakati  aligongana na beki wa Arsenal David Luiz kwenye Uwanja wa Emirates mnamo Novemba. Mchezaji huyo wa miaka 29 amejiunga na kikosi cha Mexico kabla ya mechi ya kirafiki ya Jumamosi na Wales huko Cardiff,.

Harambee Stars ilifanya kikao cha mazoezi  kabla ya Mashindano yao ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2022 dhidi ya Togo Jumatatu. Stars watasafiri kuelekea  Lome, Togo leo  katika kumaliza  mechi yao ya mwisho ya kufuzu kwa kundi G. Kocha Jacob "Ghost" Mulee ameipongeza timu hiyo kwa kuonyesha mchezo wa hali ya juu katika mchezo wao dhidi ya Misri na pia katika mechi zingine , Kenya inasimama katika nafasi ya tatu katika Kundi G na alama nne.