Hongera! Mwanariadha Ferdinand Omanyala avunja rekodi ya Kenya kwenye mbio za mita 100

Omanyala ambaye aliibuka wa tatu kwenye kundi la kwanza alimaliza na milisekunde nne tu baada ya kiongozi Fred Kerley wa Marekani aliyemaliza kwa sekunde 9.96.

Muhtasari

•Mwanariadha Ferdinand Omanyala ambaye anapeperusha bendera ya Kenya kwenye mbio za mita 100 amevunja rekodi ya Kenya katika mbio hizo baada yake kukimbia kwa sekunde 10  kwenye hatua ya nusu fainali kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea jijini Tokyo Japan.

•Mwanariadha huyo alimaliza mbele ya Yohan Blake wa Jamaica ambaye ameorodheshwa katika nafasi ya tatu.

Ferdinand Omanyala
Ferdinand Omanyala
Image: HISANI

Mwanariadha Ferdinand Omurwa Omanyala ambaye anaipeperusha bendera ya Kenya kwenye mbio za mita 100 amevunja rekodi ya Kenya katika mbio hizo baada yake kukimbia kwa sekunde 10  tu kwenye hatua ya nusu fainali katika mashindano ya Olimpiki yanayoendelea jijini Tokyo Japan.

Omanyala ambaye aliibuka wa  tatu kwenye kundi la kwanza  alimaliza na milisekunde nne tu baada ya kiongozi  Fred Kerley wa Marekani aliyemaliza kwa sekunde 9.96.  Andre De Grasse wa Australia alimaliza katika nafasi ya pili baada ya kumaliza kwa sekunde 9.98.

Kerley na De Grasse walihitimu kuingia fainali  moja kwa moja.

Mwanariadha huyo alimaliza mbele ya Yohan Blake wa Jamaica ambaye ameorodheshwa katika nafasi ya tatu.

Omanyala hata hivyo  hakuhitimu kuingia fainali kwani wachezaji wawili pekee kwa kila kundi kwenye hatua ya nusu fainali ndio huhitimu kuingia fainali moja kwa moja.