Mayweather atoa jet yake kupeleka msaada kwa wahanga wa shambulizi la Hamas nchini Israel

Ndege yake binafsi iliyojaa vifaa kama vile chakula, maji na fulana za kujikinga dhidi ya risasi kwa ajili ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) iliarifiwa kutumwa siku moja iliyopita.

Muhtasari

• Hamas, kundi ambalo limetajwa kuwa kundi la kigaidi na Serikali ya Marekani, limedhibiti Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007.

• Shambulio hilo la kigaidi lisilo na huruma na lililoratibiwa sana limesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200 nchini Israel.

Mayweather atuma msaada kwa ndege ya kibinafsi Israel.
Mayweather atuma msaada kwa ndege ya kibinafsi Israel.
Image: Screengrab// YouTube

Bondia mwenye ufanisi mkuwbwa kutokea Marekani Floyd "Money" Mayweather amearifiwa kunyoosha mkono kwake kusaidia wale walioathiriwa na mashambulizi ya kigaidi kwa kupanga kutuma ndege yake binafsi "Air Mayweather" kwa Israeli, chaneli ya Boxing News 24 imeripoti.

Siku nne zilizopita, Mayweather aliungana na watu wengi mashuhuri huku akilaani vitendo vya Hamas. Katika ukurasa wake wa Instagram, Mayweather alichapisha picha ya zamani ya ziara yake ya awali ya Jerusalem na nukuu, "Nasimama na Israel dhidi ya magaidi wa Hamas."

Mayweather aliendelea kusema, “Hamas haiwawakilishi watu wa Palestina, bali ni kundi la kigaidi linaloshambulia maisha ya watu wasio na hatia! Ninasimama kwa ajili ya wanadamu wote na ninawatakia Wamarekani wote na Waisraeli na binadamu wote waliotekwa nyara warejee salama wakati wa uhalifu huu wa kutisha wa kivita.”

Katika chapisho lake la Instagram, Mayweather aliendelea kuongeza, “Huu sio wakati wa siasa. Huu ni wakati wa usalama, kwanza kabisa. Mungu Ibariki Marekani. Mungu Ibariki Israel. Mungu awabariki wanadamu.”

Wiki moja iliyopita, Hamas ilianzisha mashambulizi makubwa ya kijeshi katika ardhi ya Israel ambayo yalijumuisha ufyatuaji wa maelfu ya maroketi, na kufuatiwa na mashambulizi ya nchi kavu, angani na baharini.

Hamas, kundi ambalo limetajwa kuwa kundi la kigaidi na Serikali ya Marekani, limedhibiti Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007.

Shambulio hilo la kigaidi lisilo na huruma na lililoratibiwa sana limesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200 nchini Israel.

Mia tisa ya majeruhi hao walitokea katika ukanda huo.

Idadi ya vifo inajumuisha angalau Wamarekani ishirini na wawili.

Katika chapisho lake la hivi majuzi la Instagram, Floyd Mayweather alichapisha ngumi yenye rangi za bendera ya Israel na kauli, “Nasimama na Israel na Wayahudi duniani kote. Ninalaani chuki dhidi ya Wayahudi kwa gharama yoyote. Nasimamia Amani. Nasimamia Haki za Binadamu. Ugaidi Sio Suluhu Kamwe."

Mbali na kueleza kuunga mkono jambo hilo, bondia huyo mwenye umri wa miaka 46, Floyd Mayweather Jr, anajiandaa kutuma ndege yake binafsi iliyojaa vifaa kama vile chakula, maji na fulana za kujikinga dhidi ya risasi kwa ajili ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF).

Miezi miwili iliyopita, Mayweather alisaidia familia 70 zilizoathiriwa na moto wa msitu wa Maui. Alilipia safari za ndege, mahali pa kukaa, chakula cha kula, na mavazi ya kuvaa. Kwa mara nyingine tena, katikati ya mkasa mwingine wa kusikitisha, Mayweather anajitokeza na kuonyesha jinsi alivyo bingwa wa kweli ndani na nje ya ulingo.