Tetesi za soka Ulaya: Hali ilivyo kwenye dirisha la uhamisho Jumapili 15.08.2021

Kiungo mfaransa wa Manchester Paul Pogba, 28, atasalia Old Trafford kumalizia mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia ili ajiunge bure Real Madrid msimu ujao

Muhtasari

•Mshambuliaji wa Chelsea, 23, Muingereza Tammy Abraham amekubali kujiunga na As Roma iliyo chini ya Jose Mourinho na atasafiri jumapili hii kwenda Italia kukamilisha uhamisho huo. (Sky Sport Italia - in Italian)

•Arsenal itajaribu kupeleka ofa kwa ajili ya kiungo wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, 23, kama itashindwa kumsajili Odegaard au kiungo wa Leicester City na England James Maddison, 24

Image: HISANI

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anataka kumbakisha Harry Kane na anatarajia kueleza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 hauzwi pale atakapokutana na wawakilishi wa Manchester City Jumapili hii. (Sunday Telegraph)

Spurs inamtaka mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic kumrithi Kane, na itamsajiri kama nahodha huyo wa England, Kane atasalia London Kaskazini. Vlahovic anasakwa pia na Atletico Madrid. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Jumamosi hii Kane amekutana na meneja wa Tottenham Nuno Espirito Santo kuona kama anaweza kuwakabili Manchester City jumapili. (Sunday Telegraph - subscription required)

Mshambuliaji wa Chelsea, 23, Muingereza Tammy Abraham amekubali kujiunga na As Roma iliyo chini ya Jose Mourinho na atasafiri jumapili hii kwenda Italia kukamilisha uhamisho huo. (Sky Sport Italia - in Italian)

Image: TWITTER

Kiungo mfaransa wa Manchester Paul Pogba, 28, atasalia Old Trafford kumalizia mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia ili ajiunge bure Real Madrid msimu ujao. (Star Sunday)

Meneja wa West Ham David Moyes anasema ili kukubali kumuuza kiungo wake wa England Declan Rice, 22 anayesakwa na Chelsea na Manchester United itahitajika angalau dau la £100m. (Mail on Sunday)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Norway Erling Braut Haaland, 21 anayehusishwa na vilabu vya Manchester United, Chelsea, Manchester City, anasema ana "ndoto na Ligi ya England". Dortmund ingependa kuumuza nyota huyo kwa klabu kutoka England au Hispania kuliko Bayern Munich walionyesha nia ya kumtaka wiki iliyopita. (Sky Sports)

Burnley imeweka dau la £13.5m kwa ajili ya kumnasa beki wa kushoto wa Lyon, raia wa Ivory Coast Maxwel Cornet, 24. (LancsLive)

Image: HISANI

Kama Cornet ataondoka Lyon, kuondoka kwake kutasaidia kupatikana kwa fedha za kumsajili mshambuliaji wa Liverpool raia wa Switzerland Xherdan Shaqiri, 29. (Athletic - subscription required)

Mlinda mlango wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 34, anasema hajazungumza na klabu yake kuhusu kuongeza mkataba wake unaoingia msimu wa mwisho, lakini anaongeza kwa kusema yuko " mtulivu" kuhusu suala hilo. (Mail on Sunday) 

Leicester City inahusishwa na mipango ya kumsajili mlinzi wa Bologna raia wa Japan Takehiro Tomiyasu,22 ambaye pia anasakwa na Tottenham na huenda akagharimu kati ya £17m-21m. (Corriere dello Sport - in Italian)

Mlinzi wa kibrazil David Luiz, 34, anataka kujiunga na klabu yenye malengo akitaka kucheza kwenye kiwango cha juu na wakati huu akisaka timu mpya baada ya kuondoka Arsenal hivi karibuni. Tayari amekataa ofa kutoka klabu za ligi kuu, mashariki ya kati na Amerika Kusini. (Mail on Sunday)

Image: GETTY IMAGES

Arsenal itajaribu kupeleka ofa kwa ajili ya kiungo wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, 23, kama itashindwa kumsajili Odegaard au kiungo wa Leicester City na England James Maddison, 24. (Sun on Sunday)

Real Madrid wako tayari kuongeza dau lake kwa ajili yakumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain mfaransa Kylian Mbappe, 22 mpaka £127.5m msimu huu kama klabu hiyo ya Hispania itamuuza kiungo wake Mnorway Martin Odegaard, 22, kwenda Arsenal kwa ada ya £42.5m. (AS - in Spanish)

Newcastle imekua ikihusishwa na uhamisho wa mshambuliaji kinda wa United raia wa Mexico Santiago Munoz kutoka klabu ya Liga MX Santos Laguna. (ESPN Mexico - in Spanish)

Mlinzi wa Chelsea, Mmarekani Matt Miazga, 26 anajiandaa kujiunga na Alaves kwa mkopo wa mwaka mmoja. (Fabrizio Romano) 

Mlinzi wa Liverpool muingereza Ben Davies, 25 anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kuelekea Sheffield United. (Sky Sports)

Image: HISANI

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Mauro Icardi, 28, anataka kujiunga na Juventus kwa hofu ya kukosa nafasi ya kucheza pale Parc des Princes kufuatia kutua kwa muargentina mwenzake Lionel Messi, 34. (Todo Fichajes - in Spanish)

West Ham inaangalia kama inaweza kumsajili mlinzi wa Aston Villa muingereza Kortney Hause, 26. (Football Insider)