Paul Pogba afichua kukumbwa na 'depression' enzi za Mourinho

Muhtasari

• Pogba alisema kwamba alikuwa na tofauti binafsi na kocha huyo mbwatukaji, jambo lililopelekea yeye kupokonywa unaibu nahodha wa Manchester United kipindi hicho.

Aliyekuwa kocha wa United Jose Mourinho na mchezaji Paul Pogba
Aliyekuwa kocha wa United Jose Mourinho na mchezaji Paul Pogba
Image: BBC Sport

Kiungo wa kati wa timu ya Manchester United ya Uingereza, Mfaransa Paul Pogba amefunguka na kukiri kwamba aliwahi kumbwa na unyongovu na msongo wa mawazo wakati wa enzi za kocha Mreno Jose Mourinho katika klabu hiyo.

Pogba alisema kwamba alikuwa na tofauti binafsi na kocha huyo mbwatukaji, jambo lililopelekea yeye kupokonywa unaibu nahodha wa Manchester United kipindi hicho.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na BBC, Pogba, 29, alikiri kukumbwa na unyongovu mara kadha tu lakini kipindi kigumu kilikuwa wakati wa uongozi wa kocha Mourinho.

“Nimekumbwa na mfadhaiko mara nyingi katika kazi yangu, lakini hauongelei juu yake. Wakati mwingine, hujui kuwa una unyongovu, unataka tu kujitenga, kuwa peke yako, na hizi ni ishara ambazo hazidanganyi. Binafsi, ilianza nilipokuwa na Jose Mourinho huko Manchester. Unajiuliza maswali, jiulize kama una makosa, kwa sababu hujawahi kuishi nyakati kama hizi maishani mwako,” alisema Pogba.

Mchezaji huyo matata wa kiungo cha kati alisema kwamba hatqa kama wachezaji wanapata pesa nyingi lakini hilo haliwazuii kutoka kupatwa na matatizo kama hayo.

“Bila shaka, tunapata pesa nyingi na hatuwezi kulalamika, kwa kweli, lakini haikuzuii kupitia nyakati hizi. Kama kila mtu maishani, nyakati zingine ni ngumu zaidi kuliko zingine,” alisema Pogba.

Alisemqa kwamba wachezaji wengi hupitia mtihani wa unyongovu na msongo wa mawazo lakini wachache sana huzungumzia suala hilo, amgalau peupe kwa umma.

“Kwa kawaida, utaisikia katika mwili wako, katika akili yako, na unaweza kujisikia vibaya kwa mwezi au hata mwaka. Lakini huwezi kusema. Angalau hadharani. Kila kitu kiko akilini mwako, akili yako inadhibiti kila kitu na kila mwanariadha wa kiwango cha juu hupitia wakati huu, lakini ni wachache tu wanaozungumza kulihusu,” alisema Pogba.