Aliyekuwa kocha wa Wolves na Spurs apata kazi ya ukocha Saudia

Nuno aliteuliwa kuwa mrithi wa Mourinho kule Hotspurs lakini kibarua chake kikaota nyasi baada ya miezi michache.

Muhtasari

• Nuno akiwa kocha mkuu wa Wolves alisaidia timu hiyo kumaliza nambari saba kwenye jedwali kwa mara zaidi ya moja.

Kocha Nuno Espirito Santo na mmiliki wa klabu ya Al Ittihad
Fabrizio Romano Kocha Nuno Espirito Santo na mmiliki wa klabu ya Al Ittihad
Image: Facebook

Baada ya kukaa nje kwenye kijibaridi kwa zaidi ya mwaka mmoja, hatimaye aliyekuwa kocha mkuu wa Tottenham Hotspurs kutokea Uingereza, Mreno Nuno Espirito Santo amepata kibarua chenye mshahara mnono.

Kocha huyo ambaye kwa wakati mmoja aliwahi kuifunza timu ya Wolves kabla ya kuigura na kuingia Spurs alijipata pabaya kikazi baada ya timu ya Spurs kuvurunda katika matokeo na kujipata pabaya katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Nuno Espirito Santo amefanikiwa kupata kazi katika timu moja kutokea Saudia kwa jina Al Ittihad kama kocha mkuu.

Santo aliingia kwenye mkataba na miamba hao wa taifa hilo la jangwani na atakuwa anawanoa makali hadi mwaka 2024.

Santo ana uzoefu mkubwa kama kocha kwani kabla ya kutimba Uingerezea kuvitumikia vilabu vya Wolves na Tottenhma, aliwahi noa makali ya vilabu vya Valencia kutoka Uhispania na Porto ya nyumbani kwao Ureno.

Mkufunzo huyo jina lake halitawahi futika katika kumbukumbu za mashabiki ugani Molineux ambapo aliisaida Wolves kuwa tishio kwa baadhi ya timu kubwa kwenye ligi kuu ya EPL, kando na kusaidia timu hiyo kumaliza ligi katika nafasi ya saba kwenye jedwali kwa zaidi ya mara moja.

Kila la kheri Nuno katika kibarua chako kipya!