RB Salzbug wakejeli uwezekano wa kununua Ronaldo, "Atakuwa mshambuizi wa 8"

Shabiki mmoja alikuwa amependekeza wamnunua Ronaldo Januari na wakajibu kwamba hawamhitaji hata kidogo.

Muhtasari

• Kejeli hizi ziliwakera watu wengi ambao walishtumu klabu hiyo kwa kusema kwamba Ronaldo ni mkubwa kumliko.

Salzburg wakejeli uwezekano wa kumnunua Ronaldo
Salzburg wakejeli uwezekano wa kumnunua Ronaldo
Image: Twitter, Facebook

Klabu ya RB Salzburg inayoshiriki ligi kuu ya nchini Austria imetoa tamko la kejeli kwa kiungo mshambuliaji wa Ureno na Manchester United, Christiano Ronaldo.

Katika tamko hilo ambalo limewaudhi maelfu ya mashabiki wa Ronaldo, shabiki mmoja kwenye mtandao wa Twitter alikuwa ametoa pendekezo kwa RB Salzburg kumnunua Ronaldo katika majira ya uhamisho mwezi Januari.

Jibu la klabu hiyo kwa pendekezo hilo lilikuwa la kejeli mno ambapo walijibu kwamba hawana haja na Ronaldo na kusema endapo watamnunua basi nafasi yake katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo itakuwa ya nane!

“Nunua Ronaldo Januari,” shabiki huyo kwa jina Vishwajeet Shukla alipendekeza.

“Atakuwa chaguo letu la nane katika safu ya ushambuliaji,” RB Salzburg walijibu huku wakimalizia kwa emoji za vicheko.

Hivi majuzi Ronaldo aliondolewa kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza na Kocha Mkuu Erik ten Hag. Pia alifungiwa kucheza mechi ya United dhidi ya Chelsea baada ya kukataa kucheza dhidi ya Tottenham Hotspur mapema.

Kuonekana kwa nyufa pana baina yake na kocha Ten Hag huko Old Trafford kumefungua vyanzo vingi ambavyo vinakisia huenda mchezaji huyo matata yuko njiano kutafuta klabu nyingine katika msimu wa uhamisho wa wachezaji mwezi Januari.

Amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa, huku Napoli na Chelsea zikiongoza pambano hilo. Uwezekano wa kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Sporting Lisbon pia haujasazwa.