Qatar kuandaa kombe la dunia ni kosa kubwa - Sepp Blatter, aliyekuwa rais wa FIFA

Kulingana na Blatter, chaguo hilo lilikuwa baya na lilikuwa na muingiliano wa kifisadi kutoka kwa rais wa Ufaransa kipindi hicho, Nicolas Sarkozy.

Muhtasari

• Blatter alisema kwamab nafasi hiyo ilikuwa inafaa kuenda wa Marekani lakini naibu wake Michel Platini akacheza shere iliyoipa Qatar nafasi hiyo kupitia mlango wa nyuma.

SEPP BLATTER aliyekuwa rais wa FIFA
SEPP BLATTER aliyekuwa rais wa FIFA
Image: sky sports

Aliyekuwa rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Sepp Blatter sasa anadai nchi ya Qatar kupewa nafasi ya kuandaa michauno ya kombe la dunia inayotarajiwa kuanza Novemba 20 yalikuwa ni makossa makubwa na uamuzi mbaya zaidi kuwahi kutokea katika soka.

Blatter alisema haya Jumanne, siku chache tu baada ya mtandao wa Netflix kutangaza kuachia Makala yatakayotumbua majipu ya jinsi ufisadi uliendeshwa katika jopo lililokuwa likiongozwa na Blatter kuteua nchi itakayoandaa mashindano ya kombe la dunia.

Kwa mujibu wa rais wa zamani wa Fifa Sepp Blatter, ambaye amerudia kudai uamuzi huo ulitokana na shinikizo la siri la kisiasa, alisema mashindano hayo yalikabidhiwa kwa nchi hiyo ya Ghuba kwa sababu ya hatua ya rais wa FIFA naibu wake Michel Platini kuwa chini ya shinikizo kutoka kwa rais wa wakati huo wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.

"Kwangu mimi ni wazi: Qatar ni kosa. Chaguo lilikuwa baya. Wakati huo, tulikubaliana katika kamati kuu kwamba Urusi inapaswa kupata Kombe la Dunia la 2018 na USA lile la 2022. Ingekuwa ishara ya amani ikiwa wapinzani wawili wa muda mrefu wa kisiasa wangeandaa Kombe la Dunia mmoja baada ya mwingine,” Blatter alinukuliwa na jarida la The Guardian.

Alipoulizwa kwa nini Qatar ilikuwa chaguo baya, Blatter hakutaja masuala ya haki za binadamu ambayo yametanda kwenye michuano hiyo, lakini alisema:

"Ni nchi ndogo sana. Kandanda na Kombe la Dunia ni kubwa sana kwa hilo."

Blatter alisema kuwa mipango ya Fifa ilivurugwa na Platini, akidai Mfaransa huyo alikuwa muhimu katika kuelekeza kura nne kutoka nchi za Ulaya kwenda Qatar, baada ya shinikizo kutoka kwa rais Sarkozy.

“Shukrani kwa kura nne za Platini na timu yake [Uefa], Kombe la Dunia lilikwenda Qatar badala ya Marekani. Ni ukweli,” Blatter alisema kuhusu matokeo ya kura 14-8 dhidi ya Marekani.

Platini alihojiwa na maafisa wa Ufaransa mnamo 2019 kama sehemu ya uchunguzi wa mchakato wa zabuni ya 2022. Mchezaji huyo wa zamani wa Ufaransa anakiri kwamba mkutano na rais Sarkozy ulifanyika lakini akakanusha kuwepo kwa muingiliano wowote wa rais huyo katika kura za kuchagua taifa la kuandaa mashindano hayo.