Fahamu pesa ambazo Argentina itapeleka nyumbani baada ya kushinda Kombe la Dunia

Mashindano hayo yalikamilika Jumapili huku Argentina ikiibuka kuwa mshindi.

Muhtasari

•Mabingwa washindi watapata kitita cha dola milioni 42 (Ksh5.186 bilioni ) huku washindi wa pili watkipata $30m (Sh3.70 bilioni).

•Timu nyingine 16 zilizoshindwa katika hatua ya makundi zitapokea kwa usawa Sh1.11 bilioni.

Argentina waliibuka washindi wa Kombe la Dunia 2022.
Image: INSTAGRAM// LIONEL MESSI

Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka wa 2022 yalikamilika rasmi siku ya Jumapili huku timu ya taifa ya Argentina ikiibuka kuwa mshindi.

Mashindano hayo yanayotazamwa kote duniani yalishuhudia Argentina ikishinda kwa mabao 4 dhidi ya Ufaransa ambao walifanikiwa kufunga penalti mbili pekee

Kabla ya mikwaju ya penalti, mechi hiyo ilikuwa imekamilika kwa sare ya 3-3.

Mabingwa washindi watapata kitita cha dola milioni 42 (Ksh5.186 bilioni ) huku washindi wa pili watkipata $30m (Sh3.70 bilioni).

Katika kipindi cha kwanza, nyota wa Argentina, Lionel Messi na Angel Di Maria waliiweka timu hiyo ya Amerika Kusini kifua mbele kwa mabao 2-0.

Hii ilikuwa baada ya Messi kupiga mkwaju wa penalti dhidi ya Ufaransa.

Alifunga penalti hiyo dakika ya 23.

Kipindi cha pili, Wafaransa walikuja wakiwa tayari kwa mechi hiyo, huku Kolo Muani akiwashindia penalti sawa na ile aliyopewa Messi.

Penati hiyo ilifungwa na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe.

Mbappe pia alifunga bao la pili na kuifanya timu ya Ufaransa kupata sare.

Croatia, ambao walimaliza wa tatu dhidi ya Morocco Jumamosi watapewa dola 27m (Sh3.32 bilioni) huku Atlas Lions wa Morocco wakinyakua hadi $25m (Sh3.08 bilioni) kwa kumaliza nafasi ya nne.

Timu nne zilizopoteza katika hatua ya robo fainali zitapata $17m (Sh2.09 bilioni) huku $13m (Sh1.60 bilioni) zikitolewa kwa timu nane zilizoshindwa katika 16 bora.

Timu nyingine 16 zilizoshindwa katika hatua ya makundi zitapokea kwa usawa Sh1.11 bilioni.